STRAIKA
hatari wa Manchester United, Wayne Rooney, Leo Jioni hatacheza Mechi ya
Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle huko Saint James Park kwa sababu ya
kuumia kidole gumba cha Mguuni.
Maumivu hayo pia yameleta wasiwasi
mkubwa kama atakuwa fiti kwa ajili ya Mechi ya Marudiano ya Robo Fainali
ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, hapo Jumatano huko Allianz Arena, Jijini
Munich watakapoivaa tena Bayern Munich baada kutoka 1-1 Jumanne
iliyopita huko Old Trafford.
Rooney, mwenye Miaka 28, aliumia kwenye Mechi hiyo na Bayern Munich lakini alimaliza Dakika zote 90.
Rooney sasa anaungana kwenye Safu ya
Majeruhi pamoja na Straika mwingine mkubwa, Robin van Persie, ambae
aliumia Goti Mwezi uliopita walipoitandika Olympiakos Bao 3-0 kwenye UCL
na kufuzu kucheza na Bayern Munich huku Van Persie akifunga Bao zote
hizo 3.
Akiongea na MUTV, Kituo cha TV cha Man
United, Meneja wa Man United, David Moyes alisema: "Rooney amechubuka
vibaya Kidole Gumba cha Mguu. Ni tatizo kwa Mechi hii na Newcastle
lakini pia inaweza kuwa tatizo kwa Mechi huko Munich. Inabidi
tumwangalie.”
Kukosekana kwa Rooney na Van Persie kunatoa nafasi kwa Danny Welbeck na Javier Hernandez ‘Chicharito’ kupata nafasi za kucheza.
Kuhusu Robin van Persie, David Moyes amesema anaendelea vizuri na matibabu na yupo njiani kurejea Uwanjani.
Van Persie, ambae alitabiriwa atakuwa
nje ya Uwanja hadi Wiki 6, ameshazikosa Mechi dhidi ya West Ham,
Manchester City, Aston Villa na Bayern Munich.
Hapo Jana, akiongea na Wanahabari kuhusu
Mechi ya Leo na Newcastle, Moyes amesema: "Robin yupo Holland akitibiwa
na tunapata Ripoti zake kila Siku, anaendelea vizuri!"
0 comments:
Post a Comment