SHERIA ZA BUNGE LA KATIBA KUREKEBISHWA!! Unknown 00:23 Edit Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uratibu na Uhusiano, Stephen Wassira amesema sheria za bunge la katiba zitabadilishwa ili kuwapa nafasi wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kurejea bungeni Wassira alitoa kauli hiyo bungeni wakati akijibu hoja za wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuwa majadiliano ndani ya Bunge la Katiba yanakiuka Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Katika mchango wake, Mdee alisema Ukawa hawako tayari kurejea ndani ya Bunge Maalumu la Katiba Agosti, mwaka huu endapo majadiliano ya Katiba hiyo hayatajikita kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba. Hata hivyo, Wassira akijibu kauli hiyo ya Mdee na wabunge wengine waliopaza sauti kuhusu kukiukwa kwa sheria hiyo alisema: “Kama hamrudi tutatumia kanuni zile kutafuta akidi na Bunge litaendelea.” “Tusigeuze Bunge hili kuwa Bunge la Katiba… Bunge la Katiba lipo tena lipo kisheria…. Kuna watu wanageukageuka wanasema sheria ilivunjwa, lakini hawasemi kifungu gani kilivunjwa,” alisema Wassira. Wassira alisema wajumbe wa Bunge laKatiba walitunga Kanuni za Bunge hilo na miongoni mwa waliokuwa walimu wakanuni hizo alikuwa Ismail Jussa na Tundu Lissu ambao ni wajumbe wa Ukawa. Share on Facebook Share on Twitter Share on Google Plus About Unknown This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel. RELATED POSTS
0 comments:
Post a Comment