UKAWA WAMPANIA Prof HARISON MAGHEMBE LEO!!

 

SIKU moja baada ya mmoja kati mawaziri wanaotajwa kuwa mizigo, Christopher Chiza, kupata wakati mgumu kupitisha bajeti ya wizara yake ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoundwa na wabunge wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), imepania kukwamisha bajeti ya Wizara ya Maji, inayoongozwa na waziri mwingine mzigo, Profesa Jumanne Maghembe.Msimamo wa kukwamisha bajeti ya wizara hiyo ulitangazwa jana na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA).Alisema mwaka wa fedha 2013/14 unaomalizika Julai 30, serikali iliongeza bajeti ya Wizara ya Maji kufikia sh bilioni 184, lakini fedha zilizotolewa ni sh bilioni 86 tu na sh bilioni 98 hazijatolewa hadi sasa, hivyo kukwamisha miradi mingi ya maji nchini.“Kwa hali hiyo hakuna sababu yoyote ya kujadili bajeti ya maji ya mwaka 2014/15, kwani bajeti ya mwaka uliopita hajatekelezwa pamoja na viongozi wa serikali kutumia Bunge kuwadanganya wananchi, kwamba suala la maji katika maeneo mbalimbali nchini, likiwemo Jiji la Dar es Salaam litakuwa  historia,” alisema Mnyika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment