CHAMA cha Wananchi
(CUF), kitaadhimisha kumbukumbu ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji
ya wananchi wa Zanzibar na kuteswa kwa wananchi Tanzania Bara.
Taarifa hiyo iliyotolewa kwa
vyombo vya habari Dar es Salaam na Naibu Mkurugenzi Habari na
Uenezi, Abdul Kambaya, imeeleza wakati wa maadhimisho hayo, pia
yatafanyika maandamano makubwa yatakayoongozwa na Mwenyekkiti wa CUF
Taifa Prof. Ibrahim Lipumba pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali.
Maandamano hayo
yataanzia viwanja vya ofisi ya CUF Temeke na kuishia kwa Mkutano wa
hadhara kwenye viwanja vya Zakhiem Mbagala. Kaulimbiu ya mwaka huu ni
'Bila Uchaguzi huru na wa Haki 2015 Taifa linaweza likarudia historia ya
2001'.
Alisema ikiwa ni sehemu
ya kumbukumbu hiyo bendera zote za CUF siku ya kesho zitapeperushwa
nusu mlingoti ikiwa ni kuomboleza vifo vya wana-CUF na wananchi wengine
zaidi ya 70 waliouawa Zanzibar.
Alisema ni sehemu ya
kukumbuka ya mateso waliofanyiwa wana-CUF walioandamana Tanzania Bara
ikiwemo tukio la kuvunjwa mkono kwa Prof. Ibrahim Lipumba, wakati wa
maandamano hayo.
Kwa mujibu wa taarifa
hiyo, maadhimisho haya ni sehemu ya shughuli za wanaharakati wa
demokrasia kutathmini kama taifa la Tanzania linafuata misingi ya Haki
na Demokrasia.
Pia ni sehemu ya
kupanga mikakati mipya kuhakiksha Tanzania inakuwa na Demokrasia na
Uhuru wa kweli inayofuata misingi ya haki za binadamu.
Kila mwaka Chama cha
Wananchi (CUF) kimekuwa na utaratibu wa kufanya maadhimisho ya
kumbukumbu ya mateso na mauaji yaliyotokea mwaka 2001 Tanzania Bara na
Zanzibar.
Mateso na mauaji ya
watu hao yalifanywa na vyombo vya usalama baada ya wananchi hasa
wanachama wa CUF kuandamana kupinga matokeo batili ya Uchaguzi, Kudai
Katiba Mpya,Tume Huru ya Uchaguzi na kudai Daftari la Kudumu la
Wapigakura.
Aidha katika kuadhimisha siku hiyo, Chama kimepanga kufanya maandamano.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment