KAMATI ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Rajab Mbarouk Mohamed,
imemtaka Meya wa Jiji la Dar es Salaam Dkt.Didas Masaburi, kujiuzulu
wadhifa huo kabla ya hajawasilisha ushahidi bungeni unaoonesha alisaini
kuuzwa kwa hisa za Shirika la Usafiri Mkoa wa Dar es Salaam (UDA).
Akizungumza Dar es
Salaam katika Mkutano wa hadhara uliondaliwa na Jumuiya ya Vijana
ya Chama cha Wananchi (JUVICUF), Mwenyekiti wa LAAC Rajab Mohamed
Mbarouk, alisema Meya huyo aliihakikishia Kamati hiyo kuwa endapo
itabainika yeye alisaini uuzwaji wa hisa za UDA kwenda kwa Kampuni ya
Simon Group, basi atajiuzulu.
Alisema ana ushahidi
kamili kuwa Jiji lilifanya hivyo katika uuzwaji wa hisa hizo, lakini
haikuambulia hata shilingi moja kutokana na uuzwaji wa hisa hizo wakati
ilitakiwa kulipwa sh.bilioni tano ambapo Meya huyo alimwambia kuwa ikiwa
atakuwa na ushahidi kuwa yeye alihusika na kusaini uuzwaji wa hisa hizo
basi atajiuzulu.
"Ninasema hivi Siku za
Masaburi zinahesabika, Januari 28 mwaka huu nitawasilisha rasmi ushahidi
bungeni kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam amesaini katika uuzwaji wa
hisa za UDA kwenda kwa Kampuni ya Simon Group bila jiji kulipwa hata
shilingi moja jambo ambalo halikubaliki kwani UDA ni Shirika la Umma,
hivyo kama anataka kujiuzulu basi ajiuzulu sasa hivi kabla sijatoa
ushahidi bungeni," alisema Mbarouk.
Alisema mbali na hilo
lakini pia jiji lilianzisha mradi wa Machinjio ambapo fedha za mradi huo
zilikuwa sh. bilioni 1.7 eneo lenye ekari 80 lakini cha ajabu na cha
kusikitisha hakuna machinjio yoyote yaliyojengwa na hadi juzi akaunti
iliyowekwa fedha hizo ilikuwa na kiasi cha sh.51,000 tu badala ya
sh.bilioni 1.7.
Mbarouk ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Ole kupitia CUF aliongeza kuwa Sheria inazitaka
Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya fedha zao kwa ajili ya
Vijana na akinamama, lakini hazitengwi.
Kwa upande wake Katibu
wa JUVICUF Wilaya ya Ilala, Abdul Khomein, alisema Serikali ya CCM haina
huruma na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) vifaa ikiwemo dawa
kuuzwa kwa bei ghali.
"Sisi walemavu wa ngozi
tunaishi kwa mashaka ndani ya nchi hii; lakini Serikali ya CCM
inashindwa kushusha hata mafuta ambayo yanasaidia kuwakinga na mionzi ya
jua ambayo inauzwa kiasi cha sh.40,000 hali ambayo walemavu hao wengi
hawawezi kumudu kununua," alisema Khomein.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment