Katika kuelekea kuadhimisha siku ya ukimwi duniani, meya wa manispaa ya jiji la Arusha Bw. Gaudens Lyimo amewataka wananchi kujenga mazoea ya kupima afya zao kila wakati ili kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati ali kupokuwa mgeni rasmi katika semina ya waandishi wa habari na waathirika wa ugonjwa wa ukimwi ilio fanyika Palace Hoteli mkoani Arusha.
Bw.Lyimo amewataka wananchi kutambua kuwa ugonjwa huu ni wakwetu wote na hauna mwenyewe ikiwa ni pamoja na kuwa makini ili kutopoteza nguvu kazi ya taifa.
Kwa upande wa waathirika wa gonjwa la ukimwi bwana Lyimo amewataka kufahamu kuwa wanaweza kuishi miaka mingi endapo watafuata masharti na kujiheshimu.
Aidha Bw.Lyimo Katika kuwasaidia waathirika waliojiunga katika vikundi mbalimbali ameiomba serikali kuwa mstari wa mbele katika kutunisha mfuko utakao wawezesha kujiendeleza kwa namna moja ama nyigine katika kujikwamua kiuchumi.
Akitoa ufafanuzi zaidi juu ya takwimu ya waathirika wa ukimwi mratibu wa masuala ya ukimwi wa jiji la Arusha Bi.Blandina Mkindi amekiri kuwapo kwa ongezeko kubwa la maambukizi mapya yanayokuwa kwa kasi.
Bi.Mkindi alisema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa mwaka elfu mbili na tatu hadi elfu mbili na nne ilikuwa ni asilimia tano nukta nne, mwaka elfu mbili na saba elfu mbili na nane asilimia moja nukta sita, na mwaka elfu mbili kumi na moja elfu mbili kumi na mbili ni asilimia tatu nukta mbili.
Vile vile alizitaja sababu za kukua kwa maambukizi hayo kwa kasi kuwa ni mila na desturi, kurithi wajane na ndoa za mitaala, muingiliano wa wageni kutoka nchi jirani, watalii ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana.
Aidha ameendelea kusema kuwa kwakukosa hofu ya mungu, ulevi ulio pindukia, pamoja na ushirikishwaji duni katika masuala ya afya ya uzazi kwa wanaume limekuwa ni tatizo linalochangia kwa kiasi kubwa kuwapo kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Hata hivyo Bi. Blandina amesema upo mkakati wa miaka mitatu utakaokuwa na lengo la kutokomeza ukimwi nchini.
Na virginia daniel.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment