FAINALI ZA KOMBE LA CAPITAL ONE KUFANYIKA VIWANJA VYA WEMBLEY JUMAPILI KATI YA TOTTENHAM vs CHELSEA!!


CAPITAL-ONE-CUPMtanange wa Tottenham uliishia kwakutoka Sare 2-2 na Sheffield United kwenye Marudiano ya Nusu Fainali ya Capital One Cup huku timu ya Tottenham ikitinga Fainali.

Mchezo huo umeifanya Tottenham kusongambele kwa Jumla ya Mabao 3-2 baada ya ushindi katika Mechi yao ya kwanza iliyochezwa  Wiki iliyopita huko White Hart Lane, walipoifunga Sheffield United Bao 1-0 kwa  Penati iliyotolewa Dakika ya 75 baada ya Jay McEveley kuushika Mpira.

Penati hiyo ilipigwa na mchezaji Andros Townsend na kuipatia timu ya Tottenham bao lililodumu hadi dakika ya mwisho wa Mchezo. 

Aidha Juzi, Chelsea walitinga Fainali baada ya kuifunga Liverpool bao 1-0 na kutinga Fainali kwa Jumla ya Mabao 2-1. 

Hatahivyo hapo Jana, Sheffield United walifunga magoli 2 kupitia mchezaji wao Che Adams na Tottenham kupata bao kupitia Christian Eriksen.

VIKOSI VILIVYOCHEZA:
Sheffield United: Howard, Flynn, Basham, McEveley, Harris, Doyle, Baxter, Campbell-Ryce, Scougall, Murphy, McNulty.
Akiba: Alcock, Higdon, Reed, Turner, Kennedy, Adams, Kieran Wallace. 

Tottenham Hotspur: Vorm, Walker, Dier, Vertonghen, Davies, Mason, Stambouli, Lamela, Dembele, Eriksen, Kane.
Akiba: Rose, Paulinho, Soldado, Adebayor, Townsend, Fazio, Friedel. 
Refa: Mike Dean
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment