NAIBU Katibu Mkuu wa
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGU) Taifa, Kibwana Njaa,
ameitaka Serikali kuwalipa wafanyakazi deni lao la sh.biloni 17 ifikapo
Julai 31, mwaka huu kinyume chake hawatashiriki Uchaguzi Mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo ameitoa jana
wakati akizungumza na wanachama wa TALGU ambao wanafanya kazi
Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Songea Vijijini
mjini Songea.
Aidha Bw Kibwana Njaa ameyasema hayo kwenye ziara yake ya Mkoani Ruvuma yenye lengo la kujua matatizo ya wanachama wao. Alisema
deni hilo la miaka mitano limekuwa likichukuliwa na serikali kwa uzito
mdogo.
Alisema wanaamini kuwa
Serikali inaweza kulipa deni hilo, lakini inashindikana kwa sababu si
kipaumbele chake; hivyo kama haitalipa hadi Julai 31, mwaka huu basi
chama hicho kitahamasisha wafanyakazi nchi nzima kuanzia Serikali za
mitaa kugomea Uchaguzi Mkuu ujao.
“Ikifikapo Julai 31, kama
Serikali haitalipa deni hilo basi tutashiriki mgomo wa kususia
uchaguzi, kwani bila kuchukua hatua hiyo kwa nchi hii hatuwezi kufika na
viongozi ni wale wale hata huyo rais atakayechaguliwa hatuna imani naye
kama hataweza kulipa deni hilo,” alisema Njaa.
Aidha aliwataka
wanachama hao kushikamana japokuwa kwa sasa, TALGU bado ina changamoto
nyingi ikiwemo kupata mtaji wa fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanachama
wake kwa riba ndogo, kwani baadhi ya taasisi za fedha zinazowakopesha
wafanyakazi zimekuwa si rafiki kutokana na riba.
“Tumeanzisha taasisi ya
fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wetu kwa sababu tuliona
taasisi za fedha zingine si rafiki kwa kuwa zinatoa mkopo kwa wanachama
wetu kwa riba kubwa jambo ambalo linasababisha wafanyakazi kuwa na
maisha magumu kila siku,” alisema Njaa.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment