Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litatuma waangalizi wa siri kwenye
mechi za raundi ya 21 na 22 ambazo ni za mwisho kwa makundi yote ya Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) zitakazoanza kuchezwa Februari 10 mwaka huu.
Mwangalizi huyo (match assessor) atatumwa na Katibu Mkuu ambapo baada ya mechi atatuma ripoti kwake kwa hatua zaidi.
Mechi
za raundi ya 21 kundi A zitachezwa Februari 10 mwaka huu kati ya KMC na
African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani), Kurugenzi FC na African Sports
(Uwanja wa Mufindi), Majimaji na JKT Mlale (Uwanja wa Majimaji), Kimondo
FC na Friends Rangers (CCM Vwawa, Mbozi), Ashanti United na Villa Squad
(Uwanja wa Karume) na Polisi Dar na Lipuli FC (Uwanja wa Azam Complex).
Raundi
ya 22 itachezwa Februari 16 mwaka huu kwa kuzikutanisha African Lyon na
Polisi Dar (Uwanja wa Karume), Kurugenzi na Lipuli FC (Uwanja wa
Mufindi), Kimondo FC na Majimaji (CCM Vwawa, Mbozi), JKT Mlale na
Ashanti United (Uwanja wa Majimaji), Friends Rangers na African Sports
(Uwanja wa Taifa), na Villa Squad na KMC (Uwanja wa Azam Complex).
Kundi
B raundi ya 21 ni Februari 17 mwaka huu kati ya Burkina Faso na JKT
Kanembwa (Uwanja wa Jamhuri), Mwadui na Polisi Tabora (Uwanja wa
Mwadui), Polisi Dodoma na Green Warriors (Uwanja wa Jamhuri), Rhino
Rangers na JKT Oljoro (Ali Hassan Mwinyi), Panone na Polisi Mara (Uwanja
wa Ushirika), Geita Gold na Toto Africans FC (Geita).
Februari
22 mwaka huu ni JKT Kanembwa na Green Warriors (Lake Tanganyika),
Mwadui na Burkina Faso (Mwadui), Polisi Tabora na JKT Oljoro (Ali Hassan
Mwinyi), Polisi Dodoma na Panone (Uwanja wa Jamhuri), Toto Africans na
Rhino Rangers (CCM Kirumba) na Geita Gold na Polisi Mara (Geita).
Mechi
za viporo za Polisi Mara zitachezwa Februri Mosi dhidi ya JKT Kanembwa,
na Februari 5 mwaka huu dhidi ya Polisi Tabora. Mechi zote zitachezwa
kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma.
FIFA YACHUNGUZA TUHUMA ZA UPANGAJI MATOKEO
Ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) upo nchini kuchunguza tuhuma za upangaji matokeo.
Waamuzi waliosimamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) pamoja na watu wengine watahojiwa na ujumbe huo. Matokeo ya
uchunguzi huo yatatangazwa na FIFA baada ya shughuli hiyo kukamilika.
Tunaendelea
kuwahimiza wanafamilia wa mpira wa miguu wazidi kuzingatia kanuni za
maadili za TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na FIFA katika
utendaji wao. FIFA itahakikisha kuwa haki inatendeka katika uchunguzi
ambao inaufanya.
TFF YAHADHARISHA MGOGORO WA ZFA KORTINI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)l imepokea kwa masikitiko taarifa za
kuwepo tena kortini kwa kesi dhidi ya uongozi wa Chama cha Mpira wa
Miguu Zanzibar (ZFA), jambo ambalo linaweza kuathiri ushiriki wa timu za
Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na Kombe la Shirikisho.
Mwishoni
mwa mwaka jana, TFF ilihadharisha juu ya masuala ya mpira wa miguu
kupelekwa mahakamani, kwani kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za
uendeshaji mpira wa miguu ambazo zinakataza masuala ya mchezo huo
kupelekwa katika mahakama za kawaida.
Kutokana
na hali hiyo, TFF iliiandikia barua ZFA kutaka mgogoro huo uondolewe
kortini na yenyewe kuridhia kuwa tayari kupeleka ujumbe Zanzibar ili
ukutane na pande zinazohusika.
Pia
TFF ilisema timu za Tanzania Bara zisingeruhusiwa kushiriki michuano ya
Kombe la Mapinduzi 2015 iwapo kesi hiyo ingeendelea kuwepo kortini na
kutaka iondolewe bila masharti yoyote.
ZFA
iliithibitishia TFF kuwa kesi hiyo imeondolewa kortini bila masharti,
hivyo timu za Tanzania Bara kuruhusiwa kushiriki katika michuano ya
Kombe la Mapinduzi. Ni
muhimu suala hilo likashughulikiwa haraka ili kutohatarisha ushiriki wa
timu za KMKM na Polisi kwenye michuano hiyo ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment