EMBE ni tunda la mwembe ambao ni mti
wenye ukubwa wa wastani una rangi ya kijani kibichi kila wakati. Kabla ya kuzaliwa embe mti huu huwa na
maua ya rangi ya waridi hadi nyeupe katika vishada vya maua na msimu wake ni
kati ya Desemba hadi Aprili.
Tunda la embe umbo lake hutofautiana,
mengi yao huwa aidha na rangi ya kijani, manjano ama nyekundu. Embe inaweza
kuiva ikiwa mtini lakini ili kuzuia uharibifu kutoka kwa ndege na popo ambao
hula tunda hili, wakulima huamua huvuna mara tu inapokomaa kwa kuangusha ikiwa
bado haijaiva.
Utagundua kuwa embe imekomaa kwa
kuiangalia rangi kwani hubadilika kutoka rangi ya kijani hadi ya manjano au
nyekundu. Kuna aina nyingi za embe kama vile embe dodo, embe mali, embe bolibo,
embe nuka, embe kidney, embe Julie Manzano na kadhalika.
Watu wengi hupenda kula embe ikiwa
imeiva lakini ulaji wake ikiwa bado mbichi ni jambo muhimu sana kiafya. Nyama
ya tunda hili ni tamu pia ina virutubisho kwani ni chanzo cha upatikanaji wa
vitamini A na C mwilini mwa binadamu.
Embe ina kiasi cha wastani cha thiamin
na niacin na asilimia 10 hadi 20 ya sukari inayosaidia mwili iwapo mtu anakula
tunda hili. Maembe pia yanaweza kugandishwa, kukaushwa kwa jua na kuweza
kutumika siku nyingi zijazo. Maembe pia yanaweza kuwekwa kwenye
makopo viwandani ama kupikwa katika jemu na watu kutumia baada ya muda fulani.
Lakini embe pia hutumika kutengeneza
jeli, pai, achari kama Mengo pickle ambayo hupendwa na watu wengi na kwa hakika
huwa ghali kutokana na tunda lenyewe kupendwa na watu. Kuna watengenezaji wa
aiskrimu huamua kutumia tunda hili kutengeneza na wengi hupenda kutumia
kutokana na harufu yake nzuri.
Watu wengi hutumia tunda hili
kutengeneza juisi ama ikiwa yenyewe tu au kwa kuchanganya na matunda mengine. Matunda
ambayo hutumika kuchanganya na embe ni ndizi, nanasi, parachichi, zabibu, papai
na kadhalika.
0 comments:
Post a Comment