Wakili wa kujitegemea Albart Msando (kushoto )akiteta jambo na mteja wake Freeman Mbowe.baada ya Mh Mbowe kutoa ushaidi jana katika mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Hai |
Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi
wa mahakama ya wilaya ya Hai, Denis Mpelembwa ,Mbowe ameiomba mahakama
kutupilia mbali kesi hiyo yenye lengo la kumpotezea muda katika
uwajibikaji wake katika Taifa.
Awali kabla ya kuanza kwa kesi hiyo eneo la
mahakama lilijaa mamia ya wafuasi wa chama hicho kutoka jimbo la Hai
wakiongozwa na vijana wa ulinzi wa chama hicho maarufu kwa jina la
redbriged waliokuwa wamevalia sare na kuzingira eneo lote la mahakama .
Mbowe alifika mahakamani hapo majira ya saa 14:05
ambapo kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa lakini ilishindikana na kuanza
kusikilizwa majira ya saa 16:05 kutokana na uwepo wa kesi nyingine ya
wananchi kuvamia shamba la mwekezaji wa kampuni ya Tanganyika Filim
Safari.
Akiongozwa na wakili wake Albert Msando Mbowe
ambae pia ni mbunge wa jimbo la Hai alidai mahakamani hapo kuwa haoni
sababu za kumpiga kijana mwenye umri kama wa mtoto wake na kuiomba
mahakama kuifutilia mbali kesi hiyo.
Mbowe anakabiliwa na kesi ya kumshambulia mwangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Nasir Yamin, wa Jimbo la Hai
Awali Mbowe aliieleza mahakama kuwa siku ya tukio
alipata taarifa kuwa kwenye kituo cha uchaguzi cha zahanati kilichopo
kata ya Nshara kuwa kuna mtu aliyeko kwenye chumba cha kujiandikisha
kinyume cha taratibu.
0 comments:
Post a Comment