Katika makala zilizopita mengi
yaliongelewa kuhusu ujauzito na umuhimu wa mahudhurio ya kliniki. Jambo hili ni sehemu tu ya kile
kinachopaswa kufanywa ili uzazi uhesabike kuwa salama.
Katika kipindi hicho kuna wakati
mama kuhesabika kuwa amejifungua bila
kujali kwamba kiumbe hicho kiko hai au la. Makala hii itafafanua juu ya
jambo hili. Mwezi hautumiki tena siku hizi kujua umri halisi wa mimba kwa kuwa
unatofautiana kwa siku. Kinachotumika sasa ni kigezo cha wiki. Wiki haibadiliki
huwa ni siku saba.
Kwa kigezo hiki mimba huhesabika
kuwa imekamilika iwapo itafikisha umri kati ya wiki 38 na 42. Na ili kufahamu
mambo mbalimbali yanatokea wakati wa ujauzito, kipindi cha mimba hugawanywa
katika sehemu kuu tatu, kila kimoja kikiwa na wiki 14.
Hapo awali ilihesabiwa kuwa jambo
lolote litakalosababisha kiumbe kutoka kati ya wiki ya kwanza na 28 basi hii itajulikana kuwa mimba
imeharibika.
Hii ilitokana na ukweli kwamba
haihesabiwi kuwa ni kujifungua kwami ilikuwa nadra sana, kwa kiumbe hicho
chenye umri unaokadiriwa wa miezi sana, kuweza kuishi.
Lakini kutokana na maendeleo makubwa
ya sayansi kiumbe kinachotoka kikiwa hai na umri wa wiki 24, wastani wa miezi
sita, kinaweza kutunzwa na baadae kikakua na kufikia umri wa kawaida.
Hivyo mwanamke alietoa kiumbe hicho
sasa huhesabiwa kuwa amejifungua. Jambo hili kwa kiasi kikubwa hutegemeana na
huduma za afya ya uzazi katika nchi husika.
Kwa nchi zilizoendelea kuweza
kukilea kichanga kilichozaliwa kikiwa na umri wa wiki 24 na kwa kiasi kikubwa
bado ni tatizo katika nchi zetu zinazoendelea.
Huduma za kipekee huhitajika ili
kiumbe kinachozaliwa katika umri huo kiweze kuishi. Hii ni pamoja na wataalamu,
vifaa na vyumba maalumu vya kutunzia vichanga hivi.
Wako ambao hutangulia kufika vituoni
kwa ajili ya kujifungua wakati muda wa kufanya hivyo unakuwa haujawadia. Hii
huwaletea usumbufu usio wa lazima kwani hulazimika kurudi nyumbani ili kusubiri
muda muafaka.
Ni jambo la kawaida kwa mjamzito
kupata maumivu kama ya kujifungua kuanzia wiki ya 26 na kuendelea wiki ya 36
lakini haimaanishi hivyo. Pia wapo ambao huchelewa kufika vituoni kwa
kutokujua.
0 comments:
Post a Comment