Akizungumza kwenye uzinduzi huo leo Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro amewaagiza RITA kuhakikisha kuwa
wanatoa mafunzo ya kutosha kwa walimu watakaoshiriki katika zoezi la
usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa ili kusitokee matatizo ya aina
yeyote.
Dk Migiro amesema mafunzo maalumu juu ya kubaini
wanafunzi ambao hawakuzaliwa hapa nchini ili wasiweze kupatiwa vyeti
kinyume cha sharia jambo ambalo baadaye linaweza kusababisha maumivu
makubwa kwa taifa.
Amesema sheria ya nchi kwa mtoto ipo wazi kwamba
mtoto yeyote anayezaliwa hapa nchini ni lazima apatiwe cheti cha
kuzaliwa bila kubagua kuwa wazazi wake ni wa taifa gani, ila aliyezaliwa
nje ya nchi alafu cheti anataka akipate hapa nchini hiyo ni tofauti
“Kwa mujibu wa sheria mtoto anapaswa kusajiliwa
ili kupatiwa cheti ndani ya siku 90 baada ya kuzaliwa, kwani Serikali
inapanga mipango yake ya maendeleo kutokana na idadi ya watu na mahitaji
yao kwa ujumla,” amesema Dk Migiro.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko
amesema RITA inatarajia kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa
wanafunzi 155,944 katika Manispaa ya kinondoni huku zoezi hilo
likizihusisha shule za msingi 140.
Saliboko alisema vyeti vitakavyotolewa kwenye
shule hizo kupitia mkakati huu havina tofauti na vinavyotolewa katika
ofisi zao na taratibu zote zitafanyika kwa mujibu wa sheria.
“Kuwa na cheti cha kuzaliwa ni nyaraka ya msingi
ambayo kila mwananchi anayestahili anapaswa kuwa nayo kwani hutoa
uthibitisho wa mahali mtu alipozaliwani taarifa muhimu sana kabla ya
kuweza kupata huduma mbalimbali za msingi kwa binadamu,” amesema
Saliboko.
Ameongeza kuwa mkakati huo umeshaanza kutekeleza
katika manispaa ya Ilala kwa kuzishirikisha shule 105 na mpaka sasa kuna
zaidi ya wanafunzi 16,000 waliosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.
0 comments:
Post a Comment