BARAZA la Mitihani
Tanzania (NECTA)limeanza kutumia mfumo wa wastani wa Pointi (GPA) katika
upangaji wa madaraja ya ufaulu katika matokeo ya mitihani ya kidato cha
nne na sita.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, MKuu wa Idara ya Fedha na
Utawala, Daniel Mafie, alisema kwa kutumia mfumo huo itakuwa rahisi hata
kwa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Kufanya udahili kwa wanafunzi.
Alisema kutokana na
maoni ya wadau wa elimu, kuanzia mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012,
NECTA walianza kutumia mfumo wa viwango visivyobadilika.
"Kwa kutumia mfumo huu
wa viwango vya ufaulu vinavyofanana hupangwa ili viwe kipimo cha ufaulu
kwa masomo yote kila mwaka, mfumo huu mpya wa viwango vya ufaulu
visivyobadilika umewezesha watahiniwa kujua viwango vya alama
vinavyotumika kutunuku matokeo," alisema Mafie.
Aliongezea kuwa awali
mfumo wa GPA ulikuwa ukitumiwa katika mitihani ya ualimu na mtihani wa
kumaliza Elimu ya Msingi(PSLE) pekee na wakati huo madaraja ya ufaulu
katika mtihani wa kidato cha nne na sita yalikuwa yakipangwa kwa kutumia
mfumo wa jumla ya pointi.
Alisema mfumo wa jumla
ya pointi umekuwa ukitumika kuanzia Baraza lilipoanzishwa mwaka 1973
hadi julai 2014. Alisema mfumo wa ufaulu ulioneshwa kwa kutumia madaraja
manne, yaani daraja la kwanza, la pili, la tatu na nne.
Hata hivyo, alisema
kutokana na maboresho yaliyofanywa, madaraja ya ufaulu katika matokeo ya
mtihani wa kidato cha nne 2014 yamepangwa kwa kutumia mfumo wa wastani
wa pointi GPA.
Alisema mfumo wa GPA
utatumika pia katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kuanzia mwaka
2015. Vile vile alisema umewezesha kuwepo kwa mfumo wa kutunuku matokeo
wa aina moja katika ngazi zote za mafunzo kuanzia elimu ya msingi hadi
elimu ya juu. Pia alisema mfumo wa GPA ni rahisi kueleweka kwa wadau wa
kada mbalimbali kwa sababu hutoa tafsiri yenye kuonesha mtahiniwa aliye
na GPA kubwa ndiye aliye na matokeo mazuri kuliko aliye na GPA ndogo.
Hata hivyo, alisema
matokeo yaliyo katika mfumo wa wastani wa pointi kwenye cheti
yatarahisisha udahili wa watahiniwa unaofanywa na Tume ya Vyuo
Vikuu(TCU) Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE)katika ngazi za juu za
Mafunzo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment