WIMBI LAZIDI KUWATANDA VIGOGO WA ESCROW, WIKI HII KUWEKWA KIKAANGONI!!

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge

VIGOGO wa Serikali waliohusika kupokea mgawo wa fedha wa zaidi ya sh.bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow wako katika wakati mgumu wiki hii kutokana na mamilioni ya watanzania kusubiri kwa hamu utetezi watakaotoa mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kuanzia kesho.

Vigogo wanaotarajiwa kuhojiwa na Baraza hilo hilo ni pamoja na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge,aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, William Ngeleja na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.

Jana na leo ilikuwa ahojiwe aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, kutokana na tuhuma ambazo zinamkabili tofauti na watuhumiwa wa Escrow,lakini hakutokea mbele ya Baraza la Maadili kutokana na kile kilichoelezwa kuwa alitoa taarifa ya ugonjwa, hivyo atashindwa kuhudhuria kwa wiki mbili.

Kuanzia kesho ndipo wataanza kuhojiwa mfululizo vigogo hao hadi Februari 27 mwaka huu. Sakata la kuhojiwa kwa vigogo hao limevutia hisia za watu wengi, ambao wanapenda kujua majibu yao wakati wakihojiwa mbele ya Baraza, hilo linaloongozwa na Jaji Hamisi Msumi.

Sakata hilo la Escrow, ndilo lilisababisha aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof.Sospeter Muhongo, kujiuzulu huku Prof.Tibaijuka akiondolewa katika nafasi yake na Rais Jakaya Kikwete, ikiwa ni utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge.

Pamoja na kuhojiwa kwa vigogo hao, lakini pia Tume hiyo itawahoji vigogo wengine tisa ambao nao wamenufaika na mgawo huo.

Kuchotwa kwa fedha zilizokuwa katika akaunti hiyo kuliibuliwa bungeni mjini Dodoma na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila hali iliyolizamu Bunge hilo kuunda Kamati ya kuchunguza sakata hilo.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment