Tume: Leteni maoni kabla ya Agosti 31


TUME ya Mabadiliko ya Katiba imezitaka asasi, taasisi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana yaliyounda mabaraza ya Katiba kwa wanachama wake kwa ajili ya kuijadili na kuitolea maoni rasimu ya Katiba mpya, ziwasilishe maoni yao kabla ya Agosti 31, mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa tume hiyo jana, Assaa Rashid, ilisema ukomo wa tarehe wa kuwasilisha maoni hayo ni kwa mujibu wa mwongozo wa uundaji wa mabaraza ya asasi, taasisi na makundi ya watu, ulioanza kutumika Juni mosi.
Assaa alisema kuwa tume hiyo haitaongeza muda wa kupokea maoni kutoka katika makundi hayo kwa kuzingatia kuwa baada ya tarehe iliyotajwa tume itakuwa na kazi ya kuyapitia na kuyachambua kwa ajili ya kuiboresha rasimu.
Alizitaka asasi, taasisi na makundi kuwasilisha maoni yao moja kwa moja katika ofisi za tume zilizopo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Ohio au Ofisi ndogo ya Zanzibar, Mtaa wa Kikwajuni.
“Kwa mujibu wa aya Na. 4.0 ya mwongozo huo, asasi, taasisi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana yanatakiwa kuwasilisha kwa tume maoni hayo kwa njia ya randama, barua, andiko au muhtasari wa makubaliano,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment