Pamoja
na Real Madrid kufungwa hapo jana na Schalke 04 ya Ujerumani kwa magoli
4 - 3 katika mechi ya klabu barani ulaya timu hiyo imefanikiwa kuingia
robo fainali ya michuano hiyo.
Real Madrid
imenufanika na matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza ambapo iliwalaza
Schalke 04 kwa jumla ya magoli 2- 0 na hivyo kusonga mbele kwa ushindi
wa jumla ya magoli 5 - 4.
Hapo jana
Mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo alivunja rekodi kuwa
mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi katika michuano hiyo.
Ronaldo alifunga
magoli 2 kati ya matatu ya Real Madrid na kufikisha jumla ya magoli
sabini nane na hivyo kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mchezaji
wa zamani wa klabu hiyo ya Real Madrid, Raul.
Mchezaji
anayemfuatia kwa karibu kwa kufunga mengi katika michuano hiyo kwa sasa
ni Lionel Messi ambaye hadi sasa ana magoli sabini na tano kwenye
michuano hiyo.
Na katika mechi
nyingine iliyopigwa hapo jana FC Porto ya Ureno nayo imeingia hatua ya
robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuibamiza timu ya FC Basel ya
uswis kwa magoli manne kwa mtungi.
Katika mechi ya awali timu hizo zilitoka sare ya goli moja kwa moja na hivyo FC Porto kuingia robo fainali kwa jumla ya magoli
Na leo kutakuwa na
mechi nyingine za michuano hiyo ambapo Chelsea wanakaribisha Paris St
Germain ya Ufaransa katika uwanja wa Stamford Bridge huku huku Bayern
Munich wakipepetana na Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
0 comments:
Post a Comment