STAA
wa Manchester United Wayne Rooney ameapa kuongeza bidii kuirudisha Timu
yake kwenye mbio za Ubingwa huku Klabu hiyo ikiripotiwa kuanza
mazungumzo na Mawakala wa Javier Hernandez ‘Chicharito’ ili kuongeza na
kuuboresha Mkataba wake.
Hivi karibuni, baada kuanza kwa kusuasua
kwenye Ligi Kuu England, Wayne Rooney alikuwa mmoja wa wapiganaji
walioirudisha kwenye reli Man United na kuiwezesha kuwafunga Vinara wa
Ligi Arsenal Bao 1-0 Jumapili iliyopita na kuwafanya wawe Pointi 5 tu
nyuma ya Vinara hao.
Rooney amesema yuko na uchu wa kuipatia
Man United Taji la 21 la Ubingwa kwa kuanzia na Pointi 3 Jumapili
watakapocheza Ugenini na Cardiff City.
Rooney, mwenye Miaka 28, amesema: “Siku
zote nimesema Kombe muhimu kwenye Msimu wowote ni Ligi Kuu. Ndio Ligi
yenu ya Nyumbani na hiyo huamua nani bora kwa Msimu wote. Hiyo ndio
muhimu kushinda!”
WAKATI HUO HUO, Manchester United inajiandaa kufungua mazungumzo ili kumpa Mkatabampya Straika wao Javier Hernandez ‘Chicharito’ na kumthibitishia kwamba bado anahitajika hapo Old Trafford.
Hivi sasa, kwa kupewa namba, Chicharito
yupo nyuma ya Robin van Persie na Wayne Rooney ambapo pia inabidi
apigane na Danny Welbeck ili kupata nafasi.
Jambo
hilo limezua minong’ono kuwa Straika huyo kutoka Mexico anataka kuhama
huku Arsenal na Tottenham pamoja na Timu ya Spain, Atletico Madrid,
zikitajwa.
Lakini Bosi wa Man United, David Moyes, ameshatoa bayana kuwa Chicharito, mwenye Miaka 25 yupo kwenye mipango yake.
Hivi sasa inasemekana Chicharito, ambae
Mkataba wake umebakisha Miaka miwili, atapewa Mkataba mpya ambao
utaboreshwa na huenda akalipwa maradufu ya Pauni 60,000 kwa Wiki
anazolipwa sasa.
Mchezaji ambae huenda akang’oka Man
United ni Kipa Anders Lindegaard kutoka Denmark ambae ameshindwa
kumng’oa David de Gea kama Kipa Nambari Wani.
Ipo minong’ono kuwa Lindegaard huenda akaenda Italy.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 23 Novemba
1545 Everton v Liverpool
1800 Arsenal v Southampton
1800 Fulham v Swansea City
1800 Hull City v Crystal Palace
1800 Newcastle United v Norwich City
1800 Stoke City v Sunderland
2030 West Ham United v Chelsea
Jumapili 24 Novemba
1630 Manchester City v Tottenham Hotspur
1900 Cardiff City v Manchester United
Jumatatu 25 Novemba
2300 West Bromwich Albion v Aston Villa
MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Arsenal |
11 |
12 |
25 |
2 |
Liverpool |
11 |
11 |
23 |
3 |
Southampton |
11 |
10 |
22 |
4 |
Chelsea |
11 |
8 |
21 |
5 |
Man Utd |
11 |
5 |
20 |
6 |
Everton |
11 |
4 |
20 |
7 |
Tottenham |
11 |
3 |
20 |
8 |
Man City |
11 |
16 |
19 |
9 |
Newcastle |
11 |
-1 |
17 |
10 |
West Brom |
11 |
0 |
14 |
11 |
Aston Villa |
11 |
-1 |
14 |
12 |
Hull |
11 |
-5 |
14 |
13 |
Swansea |
11 |
0 |
12 |
14 |
Cardiff |
11 |
-6 |
12 |
15 |
Norwich |
11 |
-12 |
11 |
16 |
West Ham |
11 |
-2 |
10 |
17 |
Stoke |
11 |
-4 |
10 |
18 |
Fulham |
11 |
-9 |
10 |
19 |
Sunderland |
11 |
-14 |
7 |
20 |
Crystal Palace |
11 |
-15 |
4 |
0 comments:
Post a Comment