BOHARI YA MADAWA TANZANIA MSD YATOA TAARIFA KUHUSU UPATIKANAJI WA DAWA ZA ARVs NCHINI


UFAFANUZI WA UPATIKANAJI WA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA VIZURI VYA UKIMWI (ARVs) NCHINI
 
Bohari ya Dawa (MSD) inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hali ya upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKMWI ni nzuri na ni ya kuridhisha.

Kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kwakusema kuwa kumekuwepo na uhaba wa kuadimika kwa dawa za Triomune 40, Triomune 30 na Atripla. Ufafanuzi 
juu ya dawa hizi ni kama ifuatavyo:

Dawa ya Triomune 40 ambayo ina machanganyiko wa Stavudine 40mg + Lamivudine 150mg + Nevirapine 200mg ilishaondolewa kwenye mzunguko mwaka 2007/2008 kutokana na sababu za kitaalam. Mojawapo ya sababu zilizotolewa ni kuleta madhara  kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na ganzi (Peripheral neuritis).

Dawa ya Triomune 30, yenye mchanganyiko wa Stavudine 30mg + Lamivudine 150mg + Nevirapine 150mg imekuwa inatumiwa kwa wingi hadi mwanzoni mwa mwaka huu (2013).

Kwa sasa dawa zote zenye kiambata cha Stavudine zinaondolewa kwenye mzunguko  wa kutumika, kulingana na maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Dawa ya Atripla ambayo ni mchanganyiko wa Tenofovir 300mg + Emtricitabine 200mg + Evavirenz 600mg, ni mojawapo ya dawa mbadala ya zile zilizotajwa hapo juu. Dawa hizi zipo za kutosha katika kanda zote tisa za Bohari ya Dawa na usambazaji unaendelea katika vituo vya kutolea huduma kama kawaida.

Aidha, upatikanaji wa dawa za aina nyingine pia ni mzuri wa kuridhisha.

Kwa taarifa hii tunawataarifu watoa huduma hii muhimu wafike katika bohari zetu kupata dawa hizi kwa utaratibu wa kawaida.
 
Aidha taarifa hii imetolewa na  Isaya Mzoro kaimu mkurugenzi mkuu wa Bohari ya madawa Tanzania
kwa vyombo vya Habari.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment