MBUNGE
wa Viti Maalum, Cecilia Pareso (CHADEMA) ameihoji serikali na kuitaka
itoe maelezo ni hatua gani inachukua ili kuhakikisha inadhibiti upotevu
wa nyaraka mbalimbali za watumishi hatua inayosababisha usumbufu wa
kushindwa kulipwa madai yao kwa wakati.
Pareso
alitoa hoja hiyo jana bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa
kuitaka serikali itoe maelezo ni kwa nini nyaraka za watumishi zinapotea
na kusababisha usumbufu kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kuchelewa
kulipwa stahiki zao.
“Serikali
inatoa kauli gani kuhusu kuwepo kwa usumbufu wa upotevu wa nyaraka za
baadhi ya watumishi hususan walimu, je serikali haioni kukosa umakini
katika utunzaji wa nyaraka hizo kunawafanya watumishi hao kukosa haki
zao kwa muda mwafaka?” alihoji Pareso.
Awali
katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Maria Hewa (CCM)
alitaka kujua serikali inadaiwa na walimu kiasi gani kwa kila mkoa na ni
lini serikali itafuta madeni hayo.
Akijibu
maswali hayo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa
Serikali za Mitaa (Elimu) Kassim Majaliwa alisema kuwa ni kweli kuna
upotevu wa nyaraka za watumishi katika halmashauri nyingi na
kuwasababishia usumbufu watumishi.
Alisema
kuwa Januari 2012 serikali ilitoa sh bilioni 19.2 za madai isiyo
mishahara na sh bilioni 25.5 za malimbikizo ya mishahara kulipa walimu
walio katika mamlaka za serikali za mitaa kwa madeni yaliyokuwepo
yamehakikiwa hadi kufikiwa Novemba 2011.
Majaliwa
pia alieleza kuwa kati ya Desemba 2012 hadi Aprili 2013 regista za
madeni ya watumishi kwa mikoa yote zinaonesha walimu 12,245 wana madai
yasiyo mishahara yanayofikia sh bilioni 8.4 ikiwemo sh milioni 519.4 kwa
walimu wa mkoa wa Mwanza.
Aidha
Naibu Waziri huyo alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2013/14 serikali
imetenga fedha za uhamisho sh bilioni 18.3 ikilinganishwa na sh bilioni
13.3 kwa mwaka 2012/13
0 comments:
Post a Comment