MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NA PEMBE YA AFRIKA.


PIX 2 829e1
Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (katikati) akizungumza na wajumbe wa RECSA (hawapo pichani) katika mkutano wao unaofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti RECSA ambapo anatarajiwa kuiongoza kwa kipindi cha miaka miwili. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Theoneste Mutsindashyaka. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. 
PIX 3 50431
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (meza kuu-kushoto) anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa Mwenyekiti anayemaliza muda wake leo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (meza kuu-katikati). 
PIX 4 2e32c
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa unaofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam kufunguliwa. Wapili kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (wakatikati). Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment