Rage ataka Yanga wahamishiwe Mabwepande.

rage 6e1d0
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick kuhakikisha anawahamisha watani zao Yanga katika eneo la Jangwani kwa kuwa ni hatarishi kwa maisha yao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Nani Mtani Jembe jijini Dar es Salaam jana, Rage mbali ya kumsifu Sadick kwa kuwaondoa baadhi ya watu na kuwapeleka Mabwepande, anamuomba awaondoe na Yanga kwani ni eneo hatarishi kwa maisha yao.
Alisema, yeye kama mtani wa Yanga, hahitaji kuwapoteza watani zake, hivyo basi anamuomba ahakikishe anawaondoa katika eneo hilo kama alivyofanya kwa watu wengine.
"Mimi nitahakikisha napeleka muswada huo bungeni, kwani wale wengine walitoka, hivyo basi namuomba Mkuu wa Mkoa awaondoe na Yanga eneo hilo kwani ni hatarishi pia kama walivyoondolewa wengine," alisema Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini na kuwavunja mbavu mashabiki wa Yanga waliokuwepo katika eneo hilo.
Wakati Rage akimtaka Sadick kufanya hivyo, wiki iliyopita mkuu huyo wa mkoa aliwaruhusu Yanga kuwahamisha watu waliovamia eneo lao kwa kuwa walishawaondoa siku nyingi toka kipindi cha mafuriko, huku Manispaa ya Ilala ikiwataka kukagua mipaka na kujiridhisha kwanza.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment