
Kitendo cha kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson kumhamisha nafasi anayocheza uwanjani Wayne Rooney kilitaka kusababisha nyota huyo kutaka kuihama klabu hiyo msimu uliopita, lakini uongozi wa klabu hiyo ulikataa kumuuza.
“Kila mtu katika klabu yetu anajua nafasi
ninayotaka kucheza, kitendo cha kocha Ferguson kunichezesha nafasi
tofauti kiliniudhi, kocha alikuwa akitaka nicheze nafasi ya kiungo, mimi
sikutaka kucheza nafasi hiyo,”alisema Rooney.
Alisema “Ni kweli katika mechi nilizocheza nafasi
ya kiungo nilicheza vizuri, lakini ni wazi nilikuwa sitaki kucheza
nafasi hiyo, kwa hiyo nilimwambia kocha nataka kucheza nafasi
ninayostahili kucheza ambayo ni nafasi ya ushambuliaji, lakini kocha
akawa hataki.”
Rooney anasema,”Nafikiri jambo kama hilo
kisaikolojia lazima litakuathiri, mimi liliniathiri katika baadhi ya
mechi, najua msimu uliopita haukuwa mzuri, lakini sababu kubwa ni kwamba
katika mechi nyingi kocha alikuwa hanipangi katika nafasi niliyokuwa
nastahili kucheza.” Ingawa Rooney ameongelea sababu hizo zilizosababisha
akose furaha katika klabu ya Manchester United msimu uliopita, anasema
hakuwa na tatizo na klabu hiyo katika kipindi cha usajili msimu huu.
“Kwa kweli katika kipindi chote cha usajili msimu
huu nilikuwa nimetulia na kufurahia maisha, mke na mimi tulikuwa
tumepata mtoto mwingine,” alisema Rooney.
Alisema,”Msimu huu nimefanya kazi kwa bidii katika
klabu ya Mancheter United, niliumia kwa sababu ya kufanya kazi kwa
bidii, nina mtazamo mzuri na nataka kuwathibitishia watu kwamba mimi ni
mchezaji wa kiwango cha juu.”
Wakati wa kipindi cha usajili msimu huu, klabu ya
Manchester United ilikataa mara mbili ofa ya Chelsea kutaka kumsajili
Rooney, ambapo mchezaji huyo katika kipindi chote hicho alikaa kimya
katika kulizungumzia suala hilo.
“Nilikaa kimya na kuacha kulizungumzia suala hilo
kwa sababu nilikuwa nikijua klabu itatoa msimamo wake na ndivyo
ilivyofanya kwani ilikataa ofa za klabu zilizokuwa zikinitaka,”alisema
Rooney.
Alisema,”mimi nilizungumza na viongozi wa klabu na
kuwaachia suala hilo, sikulizungumzia suala hilo kwenye vyombo vya
habari kwa sababu nilitaka kutulia na kuweka mtazamo wangu katika soka.”
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment