Walimu 344
nchini wamefukuzwa kazi kutoka mwaka 2008 hadi mwaka huu kutokana na
makosa mbalimbali ikiwamo kuwapa mimba wanafunzi.
Hayo yalisemwa na Katibu Msaidizi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi (TSD), Christina Hape, jijini Dar es Salaam jana. Hape
alisema mwalimu anatakiwa kuwa kama mlezi wa wanafunzi, lakini suala la
kuwapa mimba linapokuja ni kosa la jinai na kwamba ni lazima wapelekwe
polisi kwa ajiri ya kuchukuliwa hatua.
Kwa upande wake, TSD pamoja na Tume ya Utumishi wa Umma wanaweza kuwafukuza kazi walimu.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2009 wamefukuzwa walimu 40,
mwaka 2009 hadi 2010 walimu 20 , mwaka 2010 hadi 2011 walimu 13 na
mwaka 2011 hadi 2012 walimu 11 walifukizwa.
Aliongeza kuwa mpaka sasa walimu 84 walifukuzwa kazi baada ya kubainika makosa yao ya kuwapa mimba wanafunzi.
Hata hivyo, alisema ugumu unakuja pale wazazi wanapokosa kutoa
ushirikiano kwa serikali kwa kutohudhuria mahakamani na kuamua
kulimaliza baada ya mtuhumiwa huyo kuwashawishi kwamba atamuoa binti
yao.
Kwa upande wa makosa ya utoro kwa mwaka 2011 hadi 2012 walimu 152 na mwaka 2012 hadi 2013 walimu 157 walifukuzwa kazi .
Alisema kwa wastani walimu wapatao 260 mpaka sasa wamefukuzwa kazi kutokana na utoro wa maeneo ya kazi.
Naibu Katibu Tume ya Utumishi wa Umma, Idara ya Utumishi wa Walimu,
Edwini Mokongoti, alisema ili kuwezesha ufanisi katika utekelezaji wa
masuala ya kiutumishi wakuu wa vyuo vya ualimu, vyuo vya maendeleo ya
jamii, wakuu wa shule na walimu wakuu wanatakiwa kuwajibika katika
kuwaelimisha walimu taratibu za masuala ya ajira katika maeneo
mbalimbali ikiwamo kupandishwa vyeo, ajira na usajili.
Alisema pia wakuu hao watashughulikia makosa madogo madogo ya kinidhamu
na kutoa adhabu, ambayo kwa mujibu wa kanuni namab 118 ya kanuni za
utumishi wa umma ya mwaka 2003 zitakuw a, onyo, kusimamisha nyongeza ya
mshahara kufidia hasara au sehemu ya hasara ambayo mtumishi
itaisababishai serikali kutokana na uzembe wake.
0 comments:
Post a Comment