Vita dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu Mali.

Wanajeshi wa Ufaransa waliopambana na waasi Kaskazini mwa nchi
Wanajeshi wa Mali na wale wa Umoja wa Mataifa wameanzisha operesheni kubwa nchini Mali, kwa mujibu wa taarifa za jeshi la Ufaransa.
Msemaji wa jeshi la Ufaransa, Kanali Gilles Jaron aliambia shirika la habari la AFP kuwa mamia ya wanajeshi wa Ufaransa wanahusika na operesheni hiyo Kaskazini mwa nchi .

Alisema kuwa Inalenga kuzuia kuibuka kwa harakati za makundi ya wapiganaji wa kiisilamu katika eneo hilo.
Mnamo siku ya Jumatano mshambuliaji wa kujitoa mhanga, alifanya shambulizi karibu na kituo cha wanajeshi wa UN na kuwaua wanajeshi wawili pamoja na raia kadhaa.
Baraza la Usalama wa UN, limesisitiza kuwa wale waliohusika na shambulizi hilo sharti wachukuliwe hatua kali huku akisisitiza kuwa anaunga mkono jeshi la kulinda amani nchini huo.
Kwa mujibu wa afisaa huyo, operesheni hii inalenga maeneo kadhaa katika majimbo matatu na itadumu kwa muda utakaohitajika kuikamilisha.
Kiongozi wa Mali wa kundi lililojitenga na al-Qaeda katika kanda hiyo, Sultan Ould Bady, alisema kuwa lilishambulia kambi hiyo kwa sababu wanajeshi wa Chad walikuwa wanashirikiana na Ufaransa.
Ufaransa ilipeleka vikosi vyake katika maeneo yaliyokuwa yanadhibitiwa na waasi Kaskazini mwa nchi mnamo mwezi Januari.
Hata hivyo waasi hao nao walichukua hatua ya kuondoka katika eneo hilo baadhi wakienda mafichoni katika maeneo ya milimani na jangwani ambako wamekuwa wakipangia mashambulizi yao ya kuvizia dhidi ya wanajeshi.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment