Waandamanaji mjini Tripoli
Mapigano mapya yamezuka mjini Tripoli Libya jana Jumamosi(16.11.2013) wakati idadi ya watu waliouawa katika mapigano wakati wa maandamano ya kupinga wanamgambo ikipanda na kufikia watu 43.
Taarifa Zaidi zinasema kuwa zaidi ya watu 450 wamejeruhiwa wakati maandamano siku ya ijumaa
yalipozusha mapigano katika mji huo mkuu baina ya makundi ya wanamgambo
ambayo yaliendelea usiku kucha , amesema waziri wa sheria Salah
al-Marghani.
Waziri mkuu Ali Zeidan, ambaye alitekwa nyara kwa muda na wanamgambo mwezi uliopita katika tukio ambalo linaelezea hali inayoongezeka ya kutokuwa na uthabiti , ametoa wito wa "kuvumiliana na kusitishwa kwa mapigano," akionya kuwa " muda unaokuja na siku zijazo zitakuwa muhimu katika historia ya nchi ya Libya".
Usiku wa Jumamosi , maafisa wa mji wa Tripoli wametangaza , "mgomo wa nchi nzima wa siku tatu katika sekta ya umma na binafsi kuanzia Jumapili" ikiwa ni jibu kutokana na ghasia hizo. Nchi hiyo imeshuhudia ongezeko la hali isiyo tulivu wakati waasi wa zamani ambao walisaidia kuuangusha kutoka madarakani utawala wa Muammar Gaddafi uliodumu miongo kadha mwaka 2011, walipuuzia madai ya serikali ya kutaka waweke silaha zao chini.
Ghasia hizo mpya zilizuka wakati waandamanaji wakiwa wamebeba bendera nyeupe walioingia mitaani katika maeneo ya majengo ya kifahari ambayo yanatumika kama kituo cha kikosi cha Misrata, kinachoundwa na wapiganaji waliokomaa kwa vita kutoka mji wa magharibi wa Misrata, na wakidai kuwa wanamgambo hao waondoke mjini humo.
Mji wa pwani wa Misrata, ulioko kilomita 200 mashariki ya mji ya Tripoli, umeshuhudia mapigano makubwa kabisa kuwahi kutokea tangu vuguvugu la maandamano ya umma ya mwaka 2011.
Kikosi cha Misrata kilishambulia kambi ya jeshi mapema jana Jumamosi(16.11.2013) , na kuzusha duru nyingine ya mapambano ambapo mtu mmoja ameuwawa na wengine wanane wamejeruhiwa, kwa mujibu wa kanali Mosbah al-Harna, kamanda wa kikosi kingine ambacho kwa kawaida kiko chini ya mamlaka ya wizara ya ulinzi.
Harna amesema wanamgambo wa kikosi cha Misrata baadaye walipora kituo hicho cha jeshi, wakichukua magari, silaha na risasi.
Ngao ya Libya
Kikosi cha "Ngao ya Libya" ambacho ni kikosi kingine cha waasi wa zamani ambacho kilikuwa chini ya udhibiti wa serikali , baadaye kilitangaza kuwa kinalidhibiti eneo la Gharghour wakati wapiganaji wa Misrata wakijitoa katika eneo hilo.
Kikosi cha Ngao ya libya katika eneo lenye matatizo la mji wa mashariki wa Benghazi nacho kilikuwa lengo la maandamano mwezi Juni ambayo pia yalisababisha umwagikaji wa damu, ambapo watu zaidi ya 30 walipoteza maisha.
Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe
Mhariri: Amina Abubakar
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
Waziri mkuu Ali Zeidan, ambaye alitekwa nyara kwa muda na wanamgambo mwezi uliopita katika tukio ambalo linaelezea hali inayoongezeka ya kutokuwa na uthabiti , ametoa wito wa "kuvumiliana na kusitishwa kwa mapigano," akionya kuwa " muda unaokuja na siku zijazo zitakuwa muhimu katika historia ya nchi ya Libya".
Mandamano yakiendelea mjini Tripoli
Maafisa watangaza mgomoUsiku wa Jumamosi , maafisa wa mji wa Tripoli wametangaza , "mgomo wa nchi nzima wa siku tatu katika sekta ya umma na binafsi kuanzia Jumapili" ikiwa ni jibu kutokana na ghasia hizo. Nchi hiyo imeshuhudia ongezeko la hali isiyo tulivu wakati waasi wa zamani ambao walisaidia kuuangusha kutoka madarakani utawala wa Muammar Gaddafi uliodumu miongo kadha mwaka 2011, walipuuzia madai ya serikali ya kutaka waweke silaha zao chini.
Ghasia hizo mpya zilizuka wakati waandamanaji wakiwa wamebeba bendera nyeupe walioingia mitaani katika maeneo ya majengo ya kifahari ambayo yanatumika kama kituo cha kikosi cha Misrata, kinachoundwa na wapiganaji waliokomaa kwa vita kutoka mji wa magharibi wa Misrata, na wakidai kuwa wanamgambo hao waondoke mjini humo.
Watu waliojeruhiwa baada ya kushambuliwa na wanamgambo
Watu wenye silaha walifyatua risasi kutoka ndani ya nyumba hizo katika
eneo la Gharghour, na kuuwa waandamanaji kadha na kusababisha wanamgambo
wa makundi mengine kushambulia kituo hicho cha wanamgambo wa Misrata,
na kuchoma sehemu ya eneo hilo.Mji wa pwani wa Misrata, ulioko kilomita 200 mashariki ya mji ya Tripoli, umeshuhudia mapigano makubwa kabisa kuwahi kutokea tangu vuguvugu la maandamano ya umma ya mwaka 2011.
Kikosi cha Misrata kilishambulia kambi ya jeshi mapema jana Jumamosi(16.11.2013) , na kuzusha duru nyingine ya mapambano ambapo mtu mmoja ameuwawa na wengine wanane wamejeruhiwa, kwa mujibu wa kanali Mosbah al-Harna, kamanda wa kikosi kingine ambacho kwa kawaida kiko chini ya mamlaka ya wizara ya ulinzi.
Harna amesema wanamgambo wa kikosi cha Misrata baadaye walipora kituo hicho cha jeshi, wakichukua magari, silaha na risasi.
Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan
Wapiganaji wengi zaidi kutoka Misrata walijaribu kuingia mjini Tripoli
kutoka upande wa mashariki, na kuzusha mapigano na wanamgambo hasimu
kabla ya mlolongo wa wanamgambo hao wa ziada kurejea nyuma kwa kilometa
kadha.Ngao ya Libya
Kikosi cha "Ngao ya Libya" ambacho ni kikosi kingine cha waasi wa zamani ambacho kilikuwa chini ya udhibiti wa serikali , baadaye kilitangaza kuwa kinalidhibiti eneo la Gharghour wakati wapiganaji wa Misrata wakijitoa katika eneo hilo.
Kikosi cha Ngao ya libya katika eneo lenye matatizo la mji wa mashariki wa Benghazi nacho kilikuwa lengo la maandamano mwezi Juni ambayo pia yalisababisha umwagikaji wa damu, ambapo watu zaidi ya 30 walipoteza maisha.
Jeshi likilinda maeneo kuzuwia wapiganaji wa Misrata kuingia mjini Tripoli
Barabara kuelekea mji wa Tripoli kutoka upande wa mashariki imefungwa ,
amesema mwandishi mmoja wa shirika la habari la AFP,na mji huo sasa uko
shwari hadi jana jumamosi, lakini shughuli nyingi za kibiashara na
maduka zimefungwa.Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe
Mhariri: Amina Abubakar
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment