MOURINHO AMKODOLEA FALCAO, ARSENAL NA BENZEMA, CHICHARITO, DZEKO, KALOU!!

RADAMEL_FALCAO2DIRISHA LA UHAMISHO litafunguliwa Januari Mosi lakini Magazeti ya Uingereza hayaachi udaku na tayari yameanza kuchapa habari za Uhamisho na kuhusisha Klabu kubwa huko England.

Kuonekana kwa Meneja wa Chelsea Jose Mourinho kwenye MechiAGUERO_n_TEVEZ ya Kirafiki kati ya Belgium na Colombia Ijumaa Usiku kumezua uvumi kuwa Mreno huyo alikuja kumtathmini Straika wa Colombia Radamel Falcao anaechezea Monaco huko France ambae katika Mechi hiyo alifunga Bao na Colombia kushinda 2-0.
Mourinho amekana habari hizo na kudai alikwenda kuwaangalia Wachezaji wake wa Chelsea wanaochezea Belgium, Kevin De CHICHARITO12Bruyne na Eden Hazard, lakini ni wachache walioamina jibu hilo hasa ukizingatia Chelsea inasuasua katika idara ya ufungaji Mabao.
Nae Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal mwenye uhaba mkubwa wa Mastraika huku Straika wake mkubwa, Olivier Giroud, akiwa na Mchezaji mmoja tu, Nicklas Bendtner, wa kuziba pengo lake akiumia au kutakiwa kupumzika, na hali hii imezua mlolongo wa wanaodaiwa kuwa walengwa wa Wenger.
Listi hiyo ya walengwa hao inadaiwa ni Karim Benzema wa Real Madrid, Javier Hernandez ‘Chicharito’ wa Manchester United, Edin Dzeko wa Manchester City na Salomon Kalou, ambae sasa yuko Lille ya France.
Nao Barcelona wamepakaziwa kuwa wanataka kumchota Sergio Aguero ili aungane na Muargentina mwenzake, Lionell Messi, kwenye Klabu hiyo.
Huko Craven Cottage, mara baada ya kutua Mholanzi Rene Meulensteen kama Kocha Mkuu na kabla akiwa Kocha wa zamani wa Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson, kunasemekana kumefungua njia kwa Wachezaji wanaokosa namba huko Old Trafford kutua Fulham kwa Mkopo Mwezi Januari na hao ni pamoja na Wilfried Zaha na Anderson.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment