WANAOHARIBU VYANZO VYA MAJI HAWATASALIMIKA,NASSARI!!

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akifafanua jambo juu ya kukabiliana na uharibifu wa vyanzo vya maji mara baada ya zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa kwenye vyanzo liliofanywa na vijana wa vijiji vya Olkung’wado,Uvizo ,Ngabobo na Ngarinanyuki ikiwa ni njia ya kutunza bonde dogo la mto Ngarinanyuki.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari amesema kuwa watu wote wanaoharibu vyanzo vya maji katika jimbo hilo hawatasalimika lazima wachukuliwe hatua kali bila kujali wadhifa wao ili kulinda vyanzo hivyo kwa ajili ya upatikanaji endelevu wa maji.
Kufuatia zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa kwenye vyanzo vya maji  vya Inteki kilichoko kijiji cha Kireeni  lililofanywa na  vijana wa jamii ya Wameru kutoka vijiji vya Olkung’wado,Uvizo ,Ngabobo na Ngarinanyuki .
Mbunge huyo amewapongeza vijana hao kwa kazi  waliyoifanya kwa kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vinalindwa kwa gharama yeyote ile .
‘Nawaunga mkono vijana kwa kazi mliyoifanya niseme kuwa yeyote anayeharibu vyanzo vya maji hatasalimika lazima tumchukulie hatua haijalishi nani yuko nyuma yake awe kiongozi au yeyote yule kwasababu maji ni  muhimu kuliko maisha ya mtu yeyote Yule” Alisema Nassari
Pia Mbunge huyo ameahidi kuchangia miti kwa ajili ya zoezi la upandaji miti katika vyanzo vilivyoharibiwa na watu.
Kwa upande wao wananchi wameeleza kuwa wamefanya zoezi hilo baada ya kuona serikali imeshindwa kulinda vyanzo hivyo kutokana na baadhi ya watu ambao hufanya shughuli za kilimo katika vyanzo hivyo na wanapokamatwa huachiwa na kurudi uraiani bila kuchukuliwa hatua za kisheria.
Steven  John mwananchi wa kata hiyo amesema kuwa Mgogoro huo ulidumu kwa muda mrefu na kukosa suluhu hivyo wananchi wameamua kuchukua hatua ili kunusuru vyanzo hivyo  kwasababu wao ni waathirika wakubwa.
Mwanakijiji Frank Nko  amesema kuwa uharibifu huo umekithiri kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hatua ya kuingilia kati baada ya kuona kuwa serikali imeshindwa kudhibiti.
Mwenyekiti wa  jumuiya ya maji bonde dogo  la Ngarinanyuki  ,Aminieli Mungure amesema kuwa  vyanzo hivyo vimekua vikiharibiwa a kukosa usimamizi hivyo wakati umefika wa jamii kuamka na kuvilinda .
“Bonde dogo la Ngarinanyuki linalisha maji safi na kumwagilia vijiji zaidi ya vinne ambavyo ni Olkung’wado,Uvizo ,Ngabobo na Ngarinanyuki uharibifu ni mkubwa kwa hatua zinazochukuliwa ikiwemo kupanda miti tunaamini uzalishaji wa maji utaongezeka na kutokua pungufu kama ilivyo sasa ”  Alisema Mungure
Cecilia Lema kutoka Ofisi ya Bonde la Kati Arusha amesema kuwa vyanzo vya maji vilivamiwa na wanakiji waliamua kuyaondoa mazao hayo na kupanda miti na kuongeza kuwa  kulinda vyanzo hivyo ni kutekeleza sheria namba 7 ya maji.
http://victorndanshau.blogspot.com/
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment