MWEKEZAJI AVAMIWA NA KUFANYIWA UHARIBIFU ARUSHA


.


MWEKEZAJI   mwenye asili ya kiasia ,Pradeep Lodhia  amevamiwa shambani kwake na kundi la  wananchi zaidi ya 60  na kufanya uharibifu mkubwa wa mali zake sambamba na kuiba vitu mbalimbali.
Aidha wananchi hao walivamia shamba la  mwekezaji huyo lijulikanalo kama Tanzania Plantation lililopo eneo la msitu wa mbogo kata ya Mbuguni  wilayani Arumeru , lenye zaidi ya hekari elfu mbili .
Akizungumza kuhusiana na tukio hilo, Meneja wa shamba hilo,Andrew Slaa alisema kuwa uvamizi huo ulifanywa juzi majira ya saa 3 usiku ambapo wananchi hao wakiwa na silaha za jadi walivamia kambi hiyo na kuanza kuvunja nyumba huku wakiharibu mali mbalimbali na kuiba fedha pamoja na simu za wafanyakazi hao.

Slaa alisema kuwa, chanzo cha uvamizi huo kimekuwa kikichochewa na baadhi ya wanasiasa akiwemo diwani wa kata ya Mbuguni , Thomas Mollel maarufu kama ‘askofu’ambao wamekuwa wakiwarubuni wananchi hao kuwa eneo hilo ni la kwao, kitendo ambacho kimekuwa kikichangia wafanyakazi wa shamba hilo kuishi kwa wasiwasi kutokana na matisho wanayopata kutoka kwa wananchi wa.

Alisema kuwa, kitendo cha kuvamiwa na wananchi hao kimewaletea hofu kubwa kwani baadhi ya wafanyakazi wanashindwa kuendelea na kazi za kulima kutokana na kuhofia maisha yao kuvamiwa wakati wowote.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shamba hilo, Pradeep Lodhia alisema kuwa , amekuwa akitoa mchango mkubwa sana kwa jamii hususani inayozunguka shamba hilo kwa kutoa ajira na hata michango mbalimbali ya kijamii ila anashangazwa na wananchi hao wanaokuja kumzunguka tena kwa kuvamia shamba lake na kufanya uharibifu mkubwa hivyo.

Lodhia alisema kuwa,wananchi hao wamekuwa wakishawishiwa na baadhi ya diwani huyo pamoja na viongozi wa vijiji, ambao wamekuwa wakisababisha wananchi hao walete fujo katika shamba hilo na hata wakati mwingine kuzuia wafanyakazi wa shamba hilo kutoendelea na kilimo kutokana na matisho mbalimbali wanayoyapata kutoka kwa wananchi hao.

“kweli mimi nasikitika sana na swala hili ,kwani wananchi hawa wamekuwa wakinirudisha nyuma sana na kusababisha mimi kupata hasara kubwa, kutokana na shughuli zangu kusimama mara kwa mara kutokana na vitisho wanavyotutolea “alisema Lodhia.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mbuguni , Thomas Mollel maarufu kama askofu akizungumzia swala hilo alisema kuwa , yeye hajawahi kumshawishi mwananchi yeyote kufanya uhalifu ,na akiwa kama diwani hawezi kuzuia midomo ya wananchi kuongea na kudai haki zao za msingi kwani kila mwananchi anaweza kuongea anachotaka yeye na hawezi kumzuia hata kidogo.

Mollel alisema kuwa,wananchi wao wenyewe wana akili zao timamu na hawawezi kusukumwa na mtu yeyote wanapodai haki zao za msingi, hivyo aliwataka kutozusha maneno kuwa yeye ndio anachochea badala yake wakae chini na wananchi hao na kuzungumzia ili kuweza kumaliza tofauti zao.

Hata hivyo juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas ili kuthubitisha tukio hilo bado zinaendelea
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment