MSANII 'LADY JAYDEE' AELEZA JUU YA UMILIKI WA EFM RADIO 93.7!!

Judith Wambura 'Lady Jaydee'
Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchin Judith Wambura 'Lady Jaydee' ameandamwa na maswali mengi juu ya maisha yake ambapo aliulizwa juu ya kuachana na mumewake lakini pia kuhusiana na kufungua kituo cha matangazo kwa njia ya sauti (Radio) na au umiliki wa EFM Radio inayo patikana kwenye masafa ya 93.7 Fm jijini Dar es Salaam.


Haya ndiyo aliyo sema kupitia account yake ya Instagram.Ulituahidi utafungua Radio mbona kimya mpaka leo? 

JIBU : "Niliandika hiyo kitu siku ya wajinga duniani, April 1, sikuwahi kuahidi. Lakini matamanio yangu ni siku moja kumiliki kituo cha radio na ikibidi hata television. Hakuna linaloshindikana, palipo na nia pana njia ''alisema Jide''

Hatahivyo mwandishi wa habari hizi hakuishia hapo, aliendelea kwakumuuliza EFM radio ni yako?  

JIBU : Hapana sio yangu, Nafikiri inadhaniwa hivyo kutokana na kila mtu ku tamani mimi niwe na radio.  

 Je!mtaniruhusu na mimi niwaulize swali?

 Kwanini mnatamani sana niwe na radio?
 
Mungu akijaalia ntakuwa nayo na hata ikibidi kituo cha televishen. Ameandika Lady JayDee.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment