Mwezeshaji wa warsha hiyo ambaye pia ni Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco, Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa
utambulisho kwa waendesha warsha ya namna ya kuandika habari za
migogoro kutoka Shirika la Search for Common Grounds (SFCG),
yanayoendelea mjini Dodoma.
Meneja
Mradi wa SFCG wilaya ya Tarime, Bwana Jacob Mulikuza, akielezea maudhui
ya warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro kwa washiriki ambao
ni waandishi wa redio za jamii kutoka Tanzania, warsha hiyo inafanyika
mjini Dodoma.
Washiriki
wa warsha wakimsikiliza Bw. Jacob Mulikuza kutoka Shirika la Search for
Common Grounds – SFCG (hayupo pichani) akielezea jambo wakati wa warsha
ya namna ya kuandika habari za migogoro inayoendelea mjini Dodoma kwa
waandishi na watangazaji wa Redio za Jamii nchini iliyofadhiliwa na
UNESCO kupitia mradi wa DEP.
Mmoja
wa washiriki akifafanua jambo katika warsha hiyo iliyojadili namna ya
kuandika habari za migogoro kutoka Shirika la Search for Common Grounds
(SFCG) yanayoendelea mjini Dodoma.
Meneja
mradi wa SFCG wilaya ya Tarime, Bwana Jacob Mulikuza, akiwapatia
maelekezo washiriki wa warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro
kuhusu namna ya uwajibikaji katika kutatua migogoro ndani ya Jamii.
Mmoja
wa washiriki Bwana Baraka kutoka ORS Fm Radio, akiwaelezea washiriki
wenzaka namna Ya kutatua fumbo lililokuwa sehemu ya kazi za Vikundi,
katika warsha ya Uandishi wa habari za Migogoro kuhusu namna ya
uwajibikaji katika kutatua migogoro ndani ya Jamii.
Mratibu
wa vyombo vya habari wa SFCG Zanzibar, Bwana Ali sultan, akielezea
kuhusu ushiriki wa SFCG huko Zanzibar katika warsha ya namna ya kuandika
habari za migogoro kwa washiriki ambao ni waandishi wa Redio za Jamii
kutoka Tanzania, warsha hiyo inayofanyika mjini Dodoma imefadhiliwa na
Shirika la UNESCO kupitia mradi wa Demokrasia na Amani (DEP) kuelekea
Uchaguzi 2015.
Meneja
Mawasiliano wa SFCG kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Bwana
Dupont Ntererwa, akielezea kuhusu ushiriki wa SFCG huko DRC katika
warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro kwa washiriki ambao ni
Waandishi wa Redio za Jamii kutoka Tanzania, warsha hiyo inayofanyika
mjini Dodoma
0 comments:
Post a Comment