Cristiano Ronaldo
Mwaka 2013 pekee, Ronaldo amefunga mabao 66 katika mechi 56 alizocheza akiwa na Real Madrid na Ureno.
Zurich, Uswisi. Wakati wote kushinda tuzo ya Ballon d’Or inatokana na ushindani wa hali ya juu nje ya uwanja kuwa nani mwenye mvuto na kipaji binafsi.
Kwa miezi kadhaa iliyopita vita ilikuwa nani anastahili kuwa mwanasoka bora kati ya nyota wawili, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Kila moja alikuwa na mtazamo wake juu ya nani anayestahili kushinda, japokuwa mwisho wa siku Cristiano Ronaldo amefanikiwa kunyakua tuzo hiyo kwa kupata kura nyingi zaidi ya wenzake.
Kwa mujibu wa matokeo, Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Mfumo wa kupiga kura unafanywa kwenye tovuti ya Fifa, kwa chaguo la kwanza ni pointi tano, pointi tatu kwa chaguo la pili na pointi moja kwa chaguo la tatu, kwa kile kichotegemewa na wengi si Messi wala Ronaldo aliyempigia kura mwenzake kuwa chaguo la kwanza.
Jambo la kushangaza ni wawili hao kutomchagua yeyote aliyekuwa kwenye orodha ya wachezaji watatu wa mwisho.
Kura hizo zilipigwa na manahodha wa timu za taifa, makocha na wanahabari wa nchi wanachama wa FIFA.
Nahodha wa Argentina na Ureno, Messi na Ronaldo waliruhusiwa kupiga kura, lakini hawakutakiwa kujipigia kura wenyewe.
Messi yeye alitoa kura zake kwa wachezaji wenzake wa Barcelona, alimpa kura ya kwanza Andres Iniesta, Xavi na Neymar.
Ronaldo yeye alimpa kura ya kwanza mshambuliaji wa Colombia na Moncao, Radamel Falcao, huku nafasi ya pili akimpa Gareth Bale pamoja na Mesut Ozil.
Messi atakuwa na jambo la kujadili na kocha wake wa timu ya taifa Alejandro Sabella, aliyempa Ronaldo pointi muhimu kwa kumchagua wa tatu, huku Messi akiwa wa kwanza na Franck Ribery.
Winga wa Bayern Munich alimaliza nafasi ya tatu, huku nahodha wa Ufaransa, Hugo Lloris na kocha wake Didier Deschamps wakimchagua Ribery kuwa wa kwanza.
Wote wawili hawakumchagua Messi, lakini Deschamps alimchagua Ronaldo katika nafasi ya pili.
Kocha wa Ureno, Paulo Bento alifanya uteuzi kwa kuangalia mbinu zaidi, kwa kumchagua Ronaldo, Falcao na Arjen Robben, akimuondoa kabisa Messi.
Kocha wa England, Roy Hodgson na nahodha Steven Gerrard walimchagua Ronaldo kama chaguo la kwanza, lakini walitofautiana baada ya hapo.
Hodgson alimchagua Zlatan Ibrahimovic nafasi ya pili na Robin van Persie wa tatu kutokana na mchango wake kwa Manchester United, wakati Gerrard alimchagua Messi wa pili na nyota wa Liverpool, Luis Suarez wa tatuIbrahimovic, ambaye alishinda tuzo ya Puskas kwa bao lake la kisigino, alimchagua Ribery, Messi na Ronaldo, huku Samuel Eto’o na Didier Drigba wenyewe wakimchagua Yaya Toure.
Pia, Wataliano Gianluigi Buffon na kocha Cesare Prandelli wote walimchagua Andrea Pirlo kuwa wa kwanza.
Kwa upande wa wanawake kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer alinyakuwa tuzo ya Fifa ya mchezaji bora wa soka kwa wanawake huku aliyekuwa kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes akinyakua tuzo ya kuwa kocha bora wa dunia.
0 comments:
Post a Comment