Wajumbe watatu wa Bunge la Katiba
ambao ni wabunge wa CCM wametofautiana na msimamo wa chama chao kwa
kuunga mkono kura ya siri itumike kuamua ibara za Rasimu ya Katiba.
Hilo lilitokea jana katika mjadala mkali baina ya wajumbe kuhusu ama matumizi ya kura za siri yatumike au kura za wazi.
Katika mjadala huo ulioonyesha mgawanyiko wa wazi,
wajumbe wengi wanaotokana CCM na ambao wamekuwa wakipigania kura za
wazi, walionekana kuwazidi kwa wingi wale wanaotaka kura za siri.
Wajumbe wa CCM ambao ni wabunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muunganom– Esther Bulaya na Profesa Juma Kapuya walijitoa
mhanga na kueleza bayana kuwa hawako tayari kuona demokrasia
ikikandamizwa kwa kulazimishwa kupiga kura za wazi. Akishangiliwa kwa
nguvu, Bulaya alisisitiza kuwa hayuko tayari kulazimishwa kupiga kura ya
wazi huku akijua kuwa utaratibu huo unamnyima uhuru wake.
“Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko. Ni
lini na wapi maamuzi magumu kama haya yalifanyika?” Alihoji mbunge huyo
wa Viti Maalumu.
Bulaya alisema hakuna sheria inayomtaka mtu
kushurutishwa kufanya uamuzi na kwamba kumtaka atoe sauti ya juu katika
kura za wazi, ni kumlazimisha kufanya kinyume na matakwa yake.
Alisema kamwe hawezi kuuza uzalendo wake kwa
kupiga kura za wazi na kwamba atapimwa kwa utashi wake kuhusu kile
anachokiamini. Kwa upande wake, Profesa Kapuya alisema namna nzuri ya
kumpa uhuru mpiga kura, ni kutomshurutisha ili afuate matakwa ya
wengine.
Alisema kura za siri ndizo zitakazowaimarisha
wajumbe na kwamba kinyume chake, kura za wazi zitawagawa na hatimaye
kutoka bungeni wakiwa vipande vipande.
Kwa upande wake, Anna Kilango Malecela aliunga mkono
‘kiaina’ kura ya siri akisema alimsikiliza Profesa Ibrahim Lipumba kwa
karibu saa nzima kupitia Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC),
akamshawishi kutokana na hoja alizozitoa.
Kwa upande wake, Anna Kilango
Malecela aliunga mkono ‘kiaina’ kura ya siri akisema alimsikiliza
Profesa Ibrahim Lipumba kwa karibu saa nzima kupitia Kituo cha
Televisheni ya Taifa (TBC), akamshawishi kutokana na hoja alizozitoa.
Mchungaji Christopher Mtikila alitumia dakika
tano kutoa somo kwa wajumbe wa Bunge hilo, kuhusu umuhimu wa kupiga kura
ya siri badala ya kura ya wazi.
“Mwenyekiti, wewe tumekuchagua kwa kura ya siri
siyo kwamba tulikuwa wajinga kuliko wenzetu, hapana! Ni democratic
civility (ustaarabu wa kidemokrasia),” alisema.
Mjumbe mwingine, Philemon Ndesamburo aliwataka
wajumbe kuacha ushabiki wa kisiasa na kwamba lazima wazingatie kwamba
wanatengeneza Katiba itakayodumu kwa miaka 50 au miaka 100 ijayo. Hata
hivyo, wajumbe, Sixtus Mapunda na Stephen Wassira wote wa CCM, walisema
kura za wazi ndiyo suluhisho la kutoa uamuzi juu ya nani anasema nini na
kwa wakati gani.
Dk. Zainabu Gama alisema baadhi ya watu wanaotaka kura za siri wametumwa au wamekula rushwa ndiyo maana hawataki kura za wazi.
Wassira alikiri kuwa CCM imeingia na msimamo ndani ya Bunge, lakini alisema hata wajumbe wengine pia wana misimamo yao.
Wajumbe 43 ‘wachomoa’
Wajumbe 43 kati ya 201 walioteuliwa na Rais Jakaya
Kikwete kushiriki katika Bunge Maalumu la Katiba hawajaripoti bungeni
hadi kufikia jana.
Hadi jana ikiwa ni siku ya kumi na moja, wajumbe
hao walikuwa hawajasajiliwa na kati ya hao ni sita tu waliotoa udhuru
katika Ofisi ya Katibu wa Bunge.
Taarifa zilisema wajumbe wengi ambao hawajafika waliteuliwa kupitia makundi ya wakulima, wafugaji na yenye malengo yanayofanana.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema:
“Ni kweli kabisa kuhusu hizo taarifa, unajua tangu Bunge limeanza mpaka hii leo (jana) wajumbe 43 hawajaripoti na maana yake ni kwamba hawajasajiliwa. Hao sita wameeleza wazi kuwa wanauguliwa na ndiyo ambao taarifa zao zipo ofisini, ila hao wengine sijui wako wapi kwa sasa.”
“Ni kweli kabisa kuhusu hizo taarifa, unajua tangu Bunge limeanza mpaka hii leo (jana) wajumbe 43 hawajaripoti na maana yake ni kwamba hawajasajiliwa. Hao sita wameeleza wazi kuwa wanauguliwa na ndiyo ambao taarifa zao zipo ofisini, ila hao wengine sijui wako wapi kwa sasa.”
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel
alisema: “Tunajua kuna wengine hawajapata ruhusa kazini, wengine wana
shughuli maalumu na wengine wameamua kutokuja tu.”
Habari hii imeandikwa na Sharon Sauwa, Daniel Mjema, Fidelis Butahe na Habel Chidawali (Dodoma) na Leon Bahati (Dar).
0 comments:
Post a Comment