WABUNGE WAITAKA SERIKALI KUWASILISHA MSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA HABARI!!

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt FENELLA MUKANGARA

Kamati za Huduma za Jamii na ile ya Maendeleo ya Jamii zimewasilisha Taarifa zake kwa kuainisha changamoto kadhaa zilizo baini ikiwemo Uboreshaji wa matangazo ya Shirika la Utangazaji nchini –TBC- ili huduma zake ziendani na taswira ya nchi. 

Wakichangia hoja za Kamati hizo wabunge wameikumbusha serikali kuwasilisha Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya habari kwa lengo la kuboresha mazingira ya waandishi wa habari nchini na kuipongeza TBC kwa kuwa na mtaalam wa lugha za alama kwenye matangazo ya bunge. 

Akijibu hoja zilizojadiliwa baada ya kuwasilishwa kwa taarifa za Kamati za Huduma za Jamii na Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt FENELLA MUKANGARA amesema Shirika la Utangazaji TANZANIA – TBC halipendelei katika matangazo yake huku akitolea mfano matangazo ya moja kwa moja ya maadhimisho ya miaka 38 ya Chama Cha Mapinduzi – CCM yaliyofanyika mkoani RUVUMA kwa kusema chama hicho kililipia gharama za matangazo hayo.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment