MUDA MREFU WA KUWASILISHWA KWA RASIMU YA KATIBA NI TATIZO KWA WAJUMBE WA KAMATI YA KATIBA!!

Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu amesema kitendo cha Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kubadilisha kanuni kwa kutoa muda zaidi wa kuwasilishwa kwa rasimu ya katiba, kinamkera.
 
Lissu alisema kitendo kama hicho ndicho kilichomfanya yeye na mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kutaka kujiuzulu mara mbili kutokana na kupingana na wajumbe wenzao.
 Lissu alisema walitaka kujiuzulu kutokana na kuchoshwa na wajumbe kwa kufikia makubaliano ndani ya vikao, lakini wakitoka nje wanarudi na mabadiliko mengine.
 
“Tulikuwa hatusongi mbele tunafanya uamuzi na kufikia makubalino, lakini wenzetu baadaye wanaenda kujadiliana upya na kuja na mapendekezo tofauti na kuturudisha nyuma,” alisema Lissu.
 
“Baada ya majadiliano yao, mimi na Jussa tuliomba tujiondoe lakini walituomba tusijiuzulu kwa masharti kuwa tunachokubaliana hawataweza kubadilisha.”
Alisema kile ambacho kimeanza kutokea sasa ni kitendo cha Mwenyekiti Sitta kubadilisha kanuni ya 47 (a) ya Bunge hilo juu ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupewa muda unaofaa kuwasilisha rasimu katika Bunge Maalumu la Katiba.
 
Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), alisema pia hata kubadilisha kanuni kwa kupokea kwanza taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye ndipo Rais Jakaya Kikwete azungumze ni jambo wanalolipinga.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment