GODBLESS LEMA AZIDI KUMWANDAMA RAISI KIKWETE!!


Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema akihutubia wakazi wa jiji la Arusha katika viwanja vya levolosi maarufu kwa jina la Samunge hivi karibuni ambapo umati wa wakazi hao ulijitokewza kwa wingi kumsikiliza mbunge huyo

WAKAZI wa jiji la Arusha wakimsikiliza kwa makini mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema alipokuwa akielezea   sababu za ukawa kujitoa katika bunge la katiba hivi karibuni na kuwataka wakazi hao watoe ushirikiano kwa wajumbe hao watakapotembelea jiji hili katika ziara zitakazofanyika nchi nzima kueleza na kushinikiza maoni ya wananchi yaheshimiwe na serikali ya ccm

 

Katika mkutano huo mh. LEMA pamoja na mambo mengine alielezea kusikiktishwa na RAISI Kikwete baada ya kuwataka wakazi wa Karatu wasiige siasa chafu za Arusha zinazoendeshwa kwa maandamano yanayoshinikizwa na lema kila linapotokea jambo linalohusu mustakabali wa maisha ya wakazi wa jiji hilo
Alisisitiza kuwa maandamano ni haki ya msingi ya kila raia wa TANZANIA ili kudai haki wanayodhani kuwa hawajapatiwa na pia ndiyo njia pekee ya kutoa sauti ya wanyonge kwa viongozi wa serikali na kudai kuwa ataendelea kuitisha maandamano ya wananchi kila mara mpaka pale ambapo serikali itawasikiliza wakazi wake wa Arusha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment