Waziri
 wa Ujenzi, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kesho atakuwa Mgeni Rasmi 
katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara 
itakayotekelezwa katika mikoa ya Ruvuma na Mtwara.
Miradi
 hiyo itahusisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kati ya 
Namtumbo na Tunduru ambayo imegawanywa katika sehemi tatu ambazo ni 
Namtumbo – Kilimasera (km 68.20), Kilimasera – Matemanga (km 58.70) na Matemanga-Tunduru (km 60.70).
Tayari
 Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ambayo inayofadhili ujenzi huo kwa 
pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), imetoa kibali kwa ujenzi
 wa sehemu mbili za kuanzia Namtumbo hadi Kilimasera na Matemanga hadi 
Tunduru. 
 Sehemu kati ya Matemanga na Kilimasera itasubiri kibali kutoka
 Benki ya Maendeleo ya Afrika ambacho pia kinatarajiwa kutoka hivi 
karibuni.
Hii ni mara ya pili kwa sehemu hiyo ya barabara kupata makandarasi. Awali kampuni ya Progressive-Higleig Joint Venture kutoka
 India ndiyo iliyokuwa imeshinda zabuni hiyo mwaka 2010 lakini baadaye 
ikasimamishwa kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya kimkataba na 
kuonyesha udhaifu katika utekelezaji wa mradi huo.
Katika hatua nyingine kesho pia utasainiwa mkataba
 wa ujenzi wa sehemu ya barabara inayoanzia Mangaka mkoani Mtwara hadi 
Nakapanya (km 70.50) katika mkoa wa Ruvuma. Vile vile utasainiwa mradi 
mwingine wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuanzia Nakapanya 
hadi Tunduru (km 66.50) utakaotekelezwa mkoani Ruvuma.
Kusainiwa
 kwa miradi hii ni faraja kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Ruvuma pamoja na 
mikoa yote ya kusini kwani barabara hiyo ni kichocheo kikubwa kwa 
shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo hayo.
Hafla
 ya utiaji saini wa miradi hiyo itafanyika kesho (Jumatatu) tarehe 17 
Februari, 2013 katika Hoteli ya Court Yard (Protea) hapa jijini Dar es 
Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi.

0 comments:
Post a Comment