Naibu
Mkurugenzi Masuala ya Wateja kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) Bw. Isaac Mrum akieleza kuhusu uhalifu wa mitandao na hatua
wanazochukua katika kukabiliana na uhalifu huo ikiwepo kutoa elimu kwa
umma kuhusu matumizi sahihi ya mitandao.Meneja
Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent
Mungy akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu matumizi
mabaya ya mawasiliano na udanganyifu katika usajili wa namba za simu za
mkononi leo Jijini Dar es Salaam.
Serikali
yawatahadharisha wananchi kuhusu matumizi mabaya ya Mawasiliano na
udanganyifu katika usajili wa namba za simu za mkononi kwa kuwa ni kosa
la jinai.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) bw.
Innocent Mungy amesema kumekuwa na watu wachache wanaotumia mawasiliano
pasipo kuzingatia sheria na kanuni.
Kumekuwa na matukio yanayoashiria
kutumika kwa mitandao ya kijamii kuleta madharambalimbali kwa watumiaji
ikiwemo utapeli,kulipiza kisasi, ugomvi,kuwaumiza wengine kwa mambo
yasiyo na ukweli na kuvuruga kwa ujumla alisema Mungy.
Akifafanua Mungy
amesema pamoja na maendeleo chanya katika Sekta ya Mawasiliano kumekuwa
na watu wachache wanaotumia simu,mitandao ya kijamii,redio,televisheni,
na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani.
Kutokana
na hali hiyo Mungy amesema kuwa TCRA inawakumbusha wananchi wote kwamba
ni kosa la jinai kutumia mawasilano vibaya kama ilivyoainishwa kwenye
sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na Posta ( EPOCA) ya mwaka 2012.
Pia
Mungy alitoa wito kwa wananchi na watumiaji wa simu za mkononi kuunga
mkono juhudi za Serikali ili wananchi wote wasajili namba za simu kwa
ajili ya
kudumisha na kuendeleza amani ,usalama na kuharakisha maendeleo
ya sekta hii na Taifa kwa ujumla.
Naye Naibu Mkurugenzi Masuala ya
Huduma kwa wateja toka mamlaka hiyo Bw. Isaac Mruma amesema ni vyema
wananchi wakazingatia matumizi sahihi ya mawasiliano kwa maslahi mapana
na Taifa.
Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) mwaka
2010, kifungu cha 131 imeainisha kuwa ni kosa la jinai kutumia au
kuwezesha kutumika kwa namba ya simu isiyosajiliwa na adhabu yake ni
faini ya shilingi laki tano (Tsh. 500,000) au kifungo cha miezi mitatu
kwa atakayekiuka sheria hii
0 comments:
Post a Comment