Wajumbe
mbalimbali kwenye bunge la katiba wameendelea kuwasha vipaza sauti vyao
kuchangia, kutoa ya moyoni kwa kujadili sura ya kwanza na ya sita huku
ishu ya serikali mbili au tatu ikizimiliki headlines zaidi.
5. ‘Tuko kwenye nafasi nzuri
sana ya kujadili hili swala, tulijadili wakati tunaheshimiana kuliko
siku tuje kulazimisha mabadiliko ambayo hatukuyapanga, tusifikie sehemu
Wazanzibari hao wanaosemwa elfu sitini ndio waingie barabarani na jeshi’
6. ‘Mwenyekiti alikuja hapa
akatutisha oooh sijui serikali tatu jeshi, Mwanajeshi atakuja atachukua
nchi… Mwenyekiti mwenyewe alikua ni Mwanajeshi akavua uniform, Nyerere
aliposema vueni uniform akavua na leo ni rais, kuna ubaya gani
Mwanajeshi akitawala kama ana akili? hakuna ubaya, wanajeshi ni ndugu
zetu’
7. ‘Hakuna tatizo lolote siku
Mwanajeshi akija kuwa Rais kwa sababu tunae Mwanajeshi Rais Kikwete na
anaendelea tu, asiweke vikwazo kwa Wanajeshi wengine ambao watakua na
tija kwa taifa hili’
8. ‘Wanasema serikali tatu
gharama, hivi kama gharama inaongezeka alafu tija inaongezeka kuna
tatizo gani? ukifanya biashara rejareja ukitaka kuwa mkubwa ni lazima
uongeze mtaji, kama huu mfumo wa serikali mbili umeshindwa kutuondolea
matatizo mwengine anasema Znz wana hiki wana kile, mbona hamsemi kama
mpaka umeme tunawalipia?? lakini sisi huku tunalia’
Zifuatazo ni kauli za mjumbe Mh. Joseph Mbilinyi ambae pia ni mbunge wa Mbeya mjini April 15 2014
1. ‘Wabunge Wakristo hii ni
kwaresma, ni kipindi cha toba… mnatumia kipindi hiki kufanya unafiki
mbele ya Wananchi mtakuja kuhukumiwa siku itakapofika, wameharibu
mchakato wakati tumeshatumia mabilioni mengi ya hela’
2. ‘Ukarabati tu wa jengo la
bunge hili ili sisi tukae zimetumika BILIONI 8.2 alafu leo kwa sababu ya
hotuba moja tu ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wote wamegeuka,
wanaharibu kabisa tunashindwa kufanya mambo ya maana, wanaacha kupanga
mkakati wa hoja wanapanga mkakati wa kuzomea, wameishiwa mikakati mpaka
wanazomea kimkakati’
3. ‘Unakutana na mbunge tena
Waziri kama rafiki yangu Mwigulu Nchemba tunataniana ananiita mzee wa
Maandamano mi namuita mzee wa kuteka, ananiambia wewe Sugu sijui unataka
serikali tatu sijui vipi na vipi, namwambia kwani hutaki kabisa
Tanganyika anasema mi nataka Tanganyika ila nataka serikali moja, sasa
kama mnataka serikali moja kwa nini uibuke kwenye hoja ya serikali
mbili?
4. ‘Kuna watu ambao wanajadili
vitu ambavyo hawaviamini na havipo kwenye mioyo yao na hao watu
wanadhamana kwenye uongozi wa taifa hili na hii ni hatari’
9. ‘Tuna serikali mbili na
hakuna aliesimama hapa akasema serikali mbili gharama zake zipi, Wizara
ngapi hapa zinapanga majengo kila siku yanatolewa furniture? serikali
tatu gharama against what? against tija? against maendeleo? against
kwenda mbele?
10. ‘Sababu akili yenu ni
fedha ndio maana mnaangalia faida kwamba ni fedha tu, hamuangalii faida
nyingine za kijamii ambazo zitaleta tija kwa taifa hili’
11. ‘Kuna hawa ndugu zangu
viongozi wa dini, tunasema hivi mara nyingi viongozi wa dini wamekosea
walipochagua kuwa upande wa dola dhidi ya matakwa ya nchi, hii imetokea
mfano ni Padri wa Rwanda, leo hii yukwapi? kwa hiyo viongozi wa dini
wawe makini wanavyoangazia haya maswala’
12. ‘Mungu
ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Zanzibar , Mungu bariki mchakato huu
wa shirikisho la Zanzibar na Tanganyika, acheni kutupiga mkwara eti
tutagawana mbao… ni heri kugawana mbao kuliko kwenda kuzinguana huko
mbele ya safari’http://victorndanshau.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment