WACHEZAJI WAWILI WA MAN UNITED HAWATACHEZA DHIDI YA BAYERN MINICH KESHO!!



Klabu ya Manchester United leo mchana imesafiri kuelekea jijini Munich kwa ajili ya kupambana na Bayern Munich katika mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora.

Katika listi ya wachezaji waliosafiri na timu hiyo jina la mshambuliaji Wayne Rooney lilikuwepo pamoja kwamba iliripotiwa anaweza asiichezee timu hiyo kesho, lakini majina ya kiungo Marouane Fellaini na mlinzi Rafael hayakuwemo katika listi ya wachezaji waliosafiri na timu kwenda Munich ikielezwa kwamba wana majeruhi na hivyo hawataichezea timu hiyo.

United tayari imewasili Ujerumani na leo jioni walifanya mazoezi katika uwanja wa Allianz Arena kujiandaa na kipute cha kesho.

Timu hizo zilitoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Old Trafford wiki iliyopita.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment