MUME WA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI FLORA MBASHA APANDISHWA KIZIMBANI!! Unknown 00:54 Edit Mume wa Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara, Emmanuel Mbasha amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa mashtaka ya ubakaji. Mfanyabiashara huyo alipandishwa kizimbani jana na kusomewa mashtaka mawili ya ubakaji. Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Mei 23 na 25, mwaka huu, eneo la Tabata Kimanga, Ilala, Dar es Salaam. Wakili Katuga alidai kuwa katika tarehe hizo, mshtakiwa alimbaka mtoto (jina linahifadhiwa), mwenye umri wa miaka 17, kinyume cha sheria. Hata hivyo, Wakili Katuga alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Ingawa dhamana ya mshtakiwa huyo ilikuwa wazi, aliswekwa mahabusu, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo yalikuwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja akiwa ni mfanyakazi wa taasisi inayotambulika, ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni kila mmoja. Hakimu Wilberforce Luhwago anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi kesho itakapotajwa kwa ajili ya kuangalia iwapo mshtakiwa amekamilisha masharti ya dhamana. Mbasha alifikishwa mahakamani hapo asubuhi akiwa amevaa shati jekundu la mikono mirefu, suruali ya rangi ya udongo na kandambili nyekundu. Mahakamani hapo alikuwa ameambatana na wanaume wawili. Wakati akisubiri kupelekwa mahabusu, saa 7:35, watu hao aliokuwa ameambatana nao walikwenda kumnunulia chakula na maji kabla ya kuongozwa na polisi kwenda kupanda basi la Magereza kuungana na mahabusu kuelekea Gereza la Keko saa 7:05. Share on Facebook Share on Twitter Share on Google Plus About Unknown This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel. RELATED POSTS
0 comments:
Post a Comment