WABUNGE WAPENDEKEZA POSHO ZOTE ZA WABUNGE ZIKATWE KODI!!


Wakichangia mjadala wa mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa taifa na makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka 2014/15, mbunge wa Ludewa Mhe Deo Filikunjombe amesema wabunge wanapata mishahara, masurufu na posho ambazo ni kubwa lakini hawalipi kodi huku mbunge   Mhe. Lugola akisisitiza mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa-brn- ni sehemu ya michepuko inayokwamisha bajeti.
Aidha kwa upande mwingine baadhi ya wabunge wamewataka wabunge kujitadhimini kama wanalipa kodi za nyumba ili wawe mfano badala ya kuwasinikiza wananchi kulipa kodi ya nyumba wakati wao hawalipi na kusisitiza sekta ya nyumba nchni inaweza kuiiingizia serikali zaidi ya trilioni moja kwa mwaka. 
Kwa mujibu wa kalenda ya serikali inaonyesha zimebaki takribani siku kumi kukamilika mwaka wa fedha wa serikali wa 2013/2014 ambapo baadhi ya wabunge wameendelea kulalamikia kutokamilika kwa fedha za miradi ya maendeleo iliyotajwa katika mwaka husika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment