UJERUMANI WATWAA KOMBE LA DUNIA KWA MARA YA NNE TANGU MASHINDANO HAYA KUANZA!!



FAINALIWC-GOLIFAINALI ZA KOMBE LA DUNIA huko Brazil Leo zimefikia tamati kwa Fainali iliyochezwa Estadio Maracana Jijini Rio de Janeiro na Germany kuibuka Mabingwa wa Dunia baada kuifunga Argentina Bao 1-0 kwa Bao la ndani ya Dakika za Nyongeza 30 la Dakika ya 113 la Mario Gotze alietokea Benchi na kuingizwa Dakika ya 88.

Hii ni mara ya kwanza kwa Nchi kutoka Ulaya kutwaa Kombe la Dunia huko Marekani ya Kusini lakini Mashabiki wa Brazil, ambao wamelikosa Kombe hilo Nyumbani kwao baada kutandikwa 7-1 na Germany kwenye Nusu Fainali, walishangilia ushindi wa Germany kwa vile Hasimu wao mkubwa ni Argentina.

Kwenye Mechi hii, aliewahi kuwa Mchezaji Bora Duniani mara lukuki, Lionel Messi, alifunikwa na kupata nafasi chache na kwenye Kipindi cha Kwanza alionekana akitapika Uwanjani, kitu ambacho humtokea mara kadhaa akicheza Mechi.

Hadi Dakika 90, Mechi hii ilikuwa Sare 0-0.
Dakika chache kabla Mechi kuanza Germany walilazimika kumbadili Kiungo wao Sami Khedira, ambae alipata maumivu ya Musuli ya Mguu wakati akipasha moto mwili, na kumwingiza Christoph Kramer, Mchezaji wa Klabu ya Borussia Monchengladbach.

Lakini nae Kramer alidumu Dakika 32 tu baada ya kuumia alipogongana na Mabeki wa Argentina kabla ya hapo na kushindwa kuendelea baada kusikia kizunguzungu na nafasi yake kuchukuliwa na Mchezaji wa Chelsea, Andre Schurrle.

Kipindi cha Kwanza Germany walitawala na kupata nafasi kadhaa lakini Argentina walionekana hatari wakishambulia kwa kushtukiza.
Argentina walipata nafasi safi kwenye Dakika ya 20 wakati Toni Kroos alipofanya makosa kwa kupiga Kichwa cha nyuma kumrudishia Kipa na Mpira kunaswa na Gonzalo Higuaian, ambae akimkabili Kipa wa Germany Manuel Neuer, alipiga fyongo na kutoa Mpira nje.

Lakini Argentina walimudu kufunga Bao kupitia Gonzalo Higuain kwenye Dakika ya 29 na kukataliwa kwa Ofsaidi ambayo ilikuwa ni ya kweli.

Nafasi kubwa kwa Germany ilikuja kabla tu ya Haftaimu wakati Kona ilipounganishwa na Benedikt Howedes kwa Kichwa na Mpira kupiga Posti.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0.


Kabla ya michuano ya leo Argentina wametwaa Kombe la Dunia Mwaka 1986 na 1990
Huku Germany wakiwawamelibeba  mara 3 Mwaka 1954, 1974 na 1990.

FAINALIWC-HIGUAIN-OFFSIDE
Kipindi cha Pili kilianza kwa Argentina kufanya mabadiliko na kumtoa Ezequiel Lavezzi na kumwingiza Sergio Aguero.

Lakini kila Timu iliendelea kukosa nafasi za wazi na nyingi zikiwaangukia Germany huku Toni Kroos akizikosa kadhaa.
Hadi Dakika 90 kwisha, Bao zilibaki 0-0.

Dakika za Nyongeza 30 zikawadia na kwenye Kipindi cha Kwanza cha muda huo, Dakika 15 za kwanza, Bao zilibaki hivyo 0-0 huku kila upande ukiendelea kupata nafasi bila kuzitumia ipasavyo.


Moja ya nafasi hizo ni ile ya Rodrigo Palacio ambapo alimzidi mbio Beki wa Germany, Matt Hummels, na kukabiliana Kipa Neur lakini akautoa Mpira nje.
Kwenye Kipindi cha Pili vuta nikuvute iliendelea na Argentina walibahatika sana pale Sergio Aguero alipompasua chini ya jicho Kiungo wa Germany Schweinsteiger kwa kutumia mkono wake lakini Refa Rizzoli kutoka Italy hakumpa Kadi Nyekundu Muargentina huyo.

Ndipo Dakika ya 113, Mario Gotze, alieingizwa kutoka Benchi kwenye Dakika ya 88 kumbadili Miroslav Klose, kuifungia Bao pekee na la ushindi baada kupokea Krosi safi kutoka kushoto ya Andre Schurrle na kuiweka gambani kabla kuachia Shuti lililompita Kipa Sergio Romero.
Fainali zijazo za Kombe la Dunia, Mwaka 2018, zitachezwa huko Urusi.

VIKOSIVilivyokuwa uwanjani:

Germany: Neuer, Howedes, Hummels, Kramer [Andre Schurrle-32’], Schweinsteiger, Ozil [Per Mertesacker-120], Klose [Götze-88'], Muller, Lahm, Kroos, Boateng
Argentina: Romero, Garay, Zabaleta, Biglia, Perez [Gago- 86'], Higuain [Palacio-78'], Messi, Mascherano, Demichelis, Rojo, Lavezzi [Sergio Aguero-45’]
REFA: Nicola Rizzoli [Italy]
KOMBE LA DUNIA
RATIBA/MATOKEO
**Saa za Bongo
MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Brazil 0 Netherlands 3
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2200
Germany 0 Argentina 0 [Dak 120, 1-0]
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro
**KWA RATIBA/MATOKEO KAMILI BOFYA: http://www.sokainbongo.com/kombe-la-dunia-brazil-2014
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment