Mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chadema, Halima Mdee
(35) pamoja na wenzake wanane wanaokabiliwa na mashtaka yakutotii amri ya Jeshi la
polisi wanatarajia kusomewa maelezo ya awali leo katika mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
Mdee ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la wanawake Chadema
{BAWACHA} pamoja na wanachama wenzake watasomewa maelezo hayo mbele ya hakimu
mkazi Janeth Kaluyenda, kwakuwa upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Rozi Moshi (45) mkazi
wa Kinondoni B,renina Peter alimaarufu kama Lufyagila mkazi wa Kinondoni
Mkwajuni,Anna Linjewile (48) mkazi wa Mbezi Luisi na Mwanne Kassim (32)
Mkazi wa Pugu Kajiungeni.
Wengine ni Sophia Fangel (28) mkazi wa Mbezi Beach, Edward
Julius (25) mkazi wa Msasani, Martha Mtiko (27) mkazi wa Mikocheni A, pamoja na
Beatu Mmari (35) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni.
Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kuwa mnamo octoba 4 mwaka huu
katika mtaa wa Ufipa bila ya kuwa na uhalali walikiuka amri halali
yakutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP) Emmanuel Tillf kwaniaba ya
jeshi la Polisi.
Vilevile washtakiwa hao inadaiwa siku hiyo katika eneo hilo kwa
pamoja walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo lakutembea kwenda Ofisi ya
Rais.
0 comments:
Post a Comment