KAMATI
Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),itafanya mkutano
maalumu kwa ajili ya kupokea taarifa na kujadili mambo mbalimbali,
ikiwemo ushirikiano mzuri ulioneshwa na Umoja wa Katiba ya
Wananchi(UKAWA)katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini
Makene, alisema mada mbalimbali zitajadiliwa na kamati hiyo itatoa
maamuzi ya nini kifanyike.
Alisema pia kikao hicho
kitapokea taarifa ya ushirikiano wa UKAWA jinsi unavyoendelea, kwani
ushirikiano huo umeonesha matumaini makubwa kwao kutokana na kuonesha
matunda mazuri katika chaguzi za serikali za mitaa.
Alisema kamati hiyo
inafanya kikao maalumu kwa ajili ya kupokea taarifa na kujadili mambo
mbalimbali kuhusu sintofahamu kuhusiana na uandikishaji wa Daftari la
Wapigakura kwa kutumia mfumo wa BBR.
Hata hivyo, alisema
katika maeneo ambayo mfumo huo umeanza kwa majaribio umeonesha udhaifu
mkubwa wa hali ya juu; hivyo umefeli kwa kiasi kikubwa.
Pia alitaja mada
nyingine zitakazojadiliwa kuwa ni pamoja na maandalizi ya upigaji kura
ya maoni kutokana na muda mfupi uliobaki kuwa mdogo.
Alisema elimu kwa
wananchi inatakiwa kutolewa miezi miwili na kuwepo muda wa kufanya
kampeni. Vile vile alisema watapokea taarifa mbalimbali kutoka kwa
wataalamu wa chama hicho, wanasheria pamoja na sekretarieti kuu ya chama
na pia itajadili kuelekea Uchaguzi Mkuu wa urais, wabunge na madiwani.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment