Bw. Kinana aliyasema
hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Magereza, Kata
ya Tomondo, Wilaya ya Dimani, Mkoa wa Magharibi, Zanzibar.
Alisema pamoja na CUF
kuunda Serikali ya Kitaifa Zanzibar, bado imeshindwa kuwasaidia wananchi
badala yake viongozi wa chama hicho wanaendekeza safari za nje ya nchi.
"Wana CUF msikubali
kudanganywa na hotuba nzuri za viongozi wenu, mtasikia hiki na kile
lakini mwisho wa siku hamna kitu, viongozi wenu wamepewa Wizara
mbalimbali tena muhimu lakini mbona hawatoi ajira wakidai kusubiri
urais, hilo haliwezekani hadi kiama.
"Mimi nadhani, Mawaziri
wa CUF walipaswa kutumia fursa hizo kujiimarisha kwa kuwatumikia
wananchi, kuwajengea shule, zahanati na kutoa ajira badala yake,
viongozi wenu kila siku wapo nje ya nchi hasa Uarabuni kwa masilahi yao,
wangeweza kutumia nafasi hiyo lakini wanataka urais," alisema Bw.
Kinana.
Aliwataka wana CCM
kuteua wagombea wanaokubalika kwenye jamii badala ya kuwapitisha
wagombea wenye nguvu za fedha kwani wakishindwa wanaunda magenge ya
kukisaliti chama.
Alisema lazima wana CCM
wakubali matokeo wanaposhindwa katika nafasi mbalimbali wanazogombea
ili kukinusuru chama kwani wapo baadhi ya wanachama ambao wakishindwa
wanakwenda kujiunga na upinzani.
"Chagueni wagombea
wanaokubalika katika jamii ambao watakuwa waadilifu, wanaowajali
wananchi na wachapa kazi, msiwachague wanaogawa fedha ambao wakishindwa
wanasema heri tukose wote, mchana wanajifanya CCM, usiku CUF," alisema.
Alisema CCM
kimejiimarisha kuendelea kushika dola kikitekeleza ilani zake kwa
vitendo tofauti na wapinzani ambao kazi yao ni kutoa ahadi hewa kwa
wananchi wanapoomba kura.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment