Awali polisi ilizuia maandamano yaliyokuwa
yamepangwa na chama hicho ya kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu
kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara
yalifanywa na vyombo vya usalama.
Akizungumza jijini leo Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya
Dar es Salaam,Simon Siro alisema wanachama waliokamatwa walikuwa 32 kati
ya hao wawili ni wanawake na 30 ni wanaume ambao wote kwa pamoja
wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano.
“Wanachama 32 akiwemo Profesa Lipumba
tunawashikilia katika kituo cha Polisi Kati kwa kufanya maandamano
ambayo hayana kibali, wote wapo hapa tunaendelea kuwahoji,”alisema Siro.
Siro alisema walipewa taarifa ya maandamano hayo
na viongozi wa chama hicho hivyo jeshi hilo liliwaandikia barua ya
kuzuia maandamano hayo kwa kuhofia fujo kutokea.
Siro alisema sababu kubwa ya kuzuia maandamano
hayo yasifanyike kwa kuwa mwaka 2001 yalifanyika maandamano batili
yaliyosababisha baadhi ya polisi na wananchi kufa.
“Jeshi la polisi likiruhusu hayo maandamano kuna
uwezekano wa kutokea fujo na hayo maandamano ya mwaka 2001 yalikuwa si
halali na kwenye maandamano hayo walikufa askari polisi,”alisema Siro.
Alisema sababu nyingine ya kuzuia maandamano hayo
ni kuwa hivi karibuni walikamatwa watu wanaojihusisha na mambo ya ugaidi
hivyo kutokana na mazingira hayo jeshi la polisi linazuia mikusanyiko
mikubwa kwa kuhofia kutokea mambo mabaya.
0 comments:
Post a Comment