MAJAMBAZI YATIKISA JIJI LA ARUSHA,YATEKA MABASI SABA YA ABIRIA NAKUPORA MALI!!

Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, wameteka mabasi saba ya abiria yanayofanya safari zake kati ya Jiji la Arusha na Nairobi, Kenya na kupora mali na fedha ambavyo thamani yake haijafahamika.Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Jeshi la polisi, mkoani Arusha llitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Mbuga Nyeupe, wilayani Longido Mkoa wa Arusha baada ya watu hao kuweka mawe barabarani na kuwamuru abiria wote kutemka mmoja baada ya mwingine, kulala chini na kuwapekua kila kitu walichokuwa nacho.DEREVA ALIYETEKWA ASIMULIAAkisimulia mkasa huo, dereva wa basi la Perfect Trans, Joseph John, alisema kuwa watu hao waliokuwa na silaha za jadi yakiwamo mashoka, mapanga na sime, waliteka mabasi hayo majira ya saa 8 usiku.“Hao jamaa walikuwa kama 50 hivi kwani waliteka magari yetu ambayo yalikuwa yamefuatana, wametuvua hadi viatu, saa yaani walipekua hadi wanawake waliamriwa kuvua nguo na kuporwa urembo wenye nakshi ya madini ya vito,” alisema John.Alisema yeye alikuwa dereva wa kwanza kufika na basi katika eneo hilo na kuwa alipoona mawe yamepangwa kati kati ya barabara, aliamua kusimama na alipokuwa akijaribu kuyakwepa, alipigwa jiwe usoni hali iliyomfanya ashindwe kukimbia.“Hata wengine walikuwa hawajafunika nyuso zao, tukio lilidumu kwa dakika zaidi ya shirini, kila walipomaliza kupekua watu wa basi moja waliwaamuru warudi ndani ya gari,” alisimulia.Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jabir Athumani, alisema baadhi ya majambazi hayo yalikuwa yakiita majina ya baadhi ya watu na kuwaamuru kutoa fedha walizokuwa nazo.“Tunaomba vyombo ulinzi na usalama vifuatilie tukio hili kwa umakini wa hali ya juu ili kuwanasa wahusika wa tukio hili,” alisema Jabir.Aidha, alililitaka Jeshi la Polisi lirudishe magari ya doria katika barabara ya Arusha–Namanga ambayo yaliondolewa Aprili mwaka jana.POLISI: TUTAZUNGUMZA LEOKamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi leo.“Hapa nipo katika majukumu mengine, sipo ofisini nitawapa taarifa za tukio lote Jumatatu (leo) mchana, naomba subiri nitafanya mkutano na vyombo vya habari na nitawapa maelezo ya tukio lote,” alisema Sabas.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment