Shuguli mbalimbali ndani ya jiji
la Arusha zikiwemo za kibiashara jana jioni na leo zimelazimika kusimama mara
baada ya mabasi ya abiria (Daladala) kugoma kubeba abiria kwa madai kuwa
utaratibu wa Ruti ndefu zilizopangwa na Sumatra ni uonevu mkubwa,
hataivyo kugoma kwa daladala hizo
pia kuliweza kuwaaathiri wanafunzi ambao wanatumia usafiri huo kwa ajili
ya kwenda mashuleni hali ambayo iliwafanya wakose masomo lakini pia
baadhi yao wafike mashuleni wakiwa wamechelewa.
Akiongea kwa niaba ya madereva
daladala ambao wamegoma dereva,Jumaa Issa alisema kuwa wanashangazwa sana
na Sumatra kuweza kuwapangia Ruti ndefu wakati bado hata abiria wa Jiji
la Arusha hawana uwezo wa kutumia hizo ruti ndefu.
Jumaa alisema kuwa kwa historia ya
mji wa Arusha abiria wanakuwepo majira ya asubuhi na jioni kwa pekee ila
kwa majira ya mchana abiria ni wachache sana sasa hali hiyo inafanya
mparangano mkubwa sana barabarani.
“ivi kwa ruti hii hapa abiria
tunawatafuta hivyo alafu ruti ndiyo hiyo ianzishwe refu bado tajiri
anataka fungu lake la fedha jioni, kama haitoshi bado hatujashikwa na
Matrafiki bado hatujala sisi na makonda wetu bado familia zetu
hazijatudai kila siku je kwa hali hiyo tutafika kweli au ndio
wanatufanya sasa tuwe majambazi tena wa kutumia Silaha”
aliendelea kwa kusema kuwa hapo
awali kulikuwa na vikao ambavyo vilifanyika lakini hakuweza kukubaliana
muafaka wa ruti ndefu ambazo Sumatra walikuwa wanazitaka kitu cha
kushangaza nikwamba tayari wameshaambiwa kuanza ruti ndefu jambo ambalo
wamelipinga.
“kama wanataka hizi ruti ndefu
basi wanatakiwa wapandishe nauli lasivyo sisi kama madereva tutateseka
sana kiasi cha kushidwa kuwafikisha abiria mahali ambapo tunatakiwa
kuwafikisha”aliongeza Jumaa.
Katika hatua nyingine akiongea kwa
niaba ya abiria Bi Neema Palangyo kutoka katika eneo la kwa Muorombo
alisema kuwa mgomo huo umesababisha madhara makubwa sana kwa wananchi wa
Arusha kwanitumepoteza pesa nyingi huku uzalishaji wa siku ukiwa mdogo kutokana na watu wengi kutokuwa katika maeneo yao ya kazi na wengine wakihofu kuzidisha matumizi pasipokujua watarudi vipi nyumbani kwao.
“hapa arusha mjini kila mtu
anategemea zaidi usafiri wa daladala ili kuweza kufika mjini sasa kama
kuna mgomo tutafikaje mimi naishauri Serikali wakati mwingine kuweza
kufanya mawasiliano ya kutosha kwani tunaoteseka ni sisi kina mama na
watoto ambao tunategemea usafiri wa jumla”aliongeza Neema.
Hataivyo zaidi ya daladala mia
tano ambazo zote zinafanya shuguli zake za usafiri jijini Arusha
ziliweza kugoma na kisha kupinga azimio hilo la ruti ndefu ambalo
lilitolewa kwa kushirikiana na wadau wote wa Sumatra na usafirishaji
Jijini Arusha.
0 comments:
Post a Comment