Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, alisema jana kuwa anawajibika kutekeleza amri hiyo kutoka ndani ya chama.
Alisema agizo hilo halina lengo baya zaidi ya
kukijenga chama ili kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kuimarisha
nidhamu miongoni mwa wanachama.
“Huwa ananituma, anaweza akaniambia nifanye au nisifanye jambo ambalo halina masilahi ya chama,” alisema Nchemba.
Utekelezaji huo umekuja baada ya Nchemba
kuandikiwa barua na Kinana ambayo pia imezagaa katika mitandao ya
kijamii ikimtaka kusitisha ziara anazozifanya maeneo mbalimbali kwa kuwa
hazina baraka za chama hicho.
Katika barua hiyo iliyoandikwa Januari 18,
ilieleza Nchemba amekuwa akifanya ziara nyingi katika mikoa na wilaya
bila ya ushirikishwaji wa makao makuu, mikoa na wilaya na hasa kamati za
siasa.
0 comments:
Post a Comment